Stevo Simple Boy asusia safari ya Saudi Arabia

Anadai kuwa kuna tatizo la mawasiliano baina yake na wakala wake aliye nchini Saudi Arabia

Muhtasari

• Stevo alifaa kusafiri tarehe 22 Septemba kuelekea Saudi Arabia kufanya tumbuizo la miziki yake.

Stevo Simple Boy
Stevo Simple Boy
Image: Stevo Simple Boy8//Facebook

Msanii Stevo Simple Boy ametishia kupangua tumbuizo aliloandaliwa nchini Saudi Arabia kwa kutumiwa tiketi ya ndege ya daraja la watu wa kawaida yaani economy class badala ya daraja la watu wa biashara.

Kulingana na mkala wa Stevo, safari ya kuelekea Saudi Arabia ilifaa kufanyika tarehe 22 lakini alisikitikia kuwa safari hiyo huenda ikakosa kufanyika.

Kulingana na msanii huyo wa kibao Vijana tuwache mihadarati, amesema kuwa wakala wa kuwaalika nchini Saudi Arabia wamekosa kutoa maelezo kamili ya safari yao.

Simple Boy amedai kuwa mbali na tiketi za ndege walizokuwa wameitisha kutoka kwa wakala aliye Saudi Arabia,pia maelezo ya hoteli watakayolala hayakutolewa.

Staa huyo aidha amesema kuwa mkataba walioweka baina yake na wenyeji wao Saudi Arabia umeshindwa kutekelezwa jambo ambalo Stevo alisema hawezi kuenda.

Stevo hata hivyo amesema kuwa pesa alizokuwa ametumiwa kama amana zingalipona kamwe hawezi kuzitumia.

Stevo amesema kuwa hawezi kuenda nchini Saudi Arabia bila mpangilio maalum kisha habari ziwepo kuwa amegwama huko.