"Mimi sio kienyeji!" Huddah amjibu Salasya baada ya kutangaza amechoka kujaribu kumtongoza

Hii ni baada ya Salasya kusema kuwa kuwa ameshindwa kuendelea kutoka nje na Huddah Monroe

Muhtasari

• Mbunge Peter Salasya awali alikiri kuwa hawezani na Huddah Monroe katika mahusiano bali anarudi kutafuta vienyeji ambao amezoea.

Huddah Monroe amefichua kuwa Salasya sio rika lake wala yeye sio kienyeji. 

Image: Hisani

Mwanasosholaiti wa Kenya Huddah Monroe amemjibu mbunge wa Mumias Mashariki Peter Salasya akimbainisha kuwa yeye sio kienyeji.

Awali mbunge Salasya  alisema kuwa amekata tamaa kuendelea kujaribu kumtongoza Huddah.

Salasya alisema kuwa hawezani na Huddah akidai kwamba serikali itaanguka.

"Mimi siwezani wataangusha serikali afadhali nirudi kwa vienyeji yangu. Najitenga rasmi kumfuata huyo msichana,"  Alisema Salasya.

Akimjibu Salasya, Huddah Monroe amemshauri Salasya kutamfuta mpenzi mwenye ni wa kiwango chake.Vile vile amemwambia kuwa yeye si kienyeji.

Monroe amekiri kuwa alitumiwa shilingi milioni mbili na mtu ambaye hakuweka jina lake wazi.

Kulingana na Huddah, hangeweza kufahamu ikiwa shilingi elfu kumi ziliingia kwenye akaunti yake kutoka kwa Salasya.

"Hakika ningewezaje kugundua shilingi 10,000! Hata sikugundua, sikuona ata,"  Alisema Huddah Monroe.

Hata hivyo, Huddah Monroe alimtaka Peter Salasya awache kumharibia jina kwa sababu ya dola themanini pekee yake.

Huddah aliweka wazi kwamba alimrudishia Mbunge Peter Salasya pesa walizokula kitoweo cha kuku.