"Naweza weka mwanamume nikiona ako na bidii na future," Sandy Kahush, muasisi wa 'kababa'

Pia alisema kuwa hataki pesa za mwanamume kwani yeye anajitengenezea na kuwa anaweza kumfanyia mwanamume wake chochote anapokuwa katika nafasi ya kumfanyia kitu.

Muhtasari

• Katika mahojiano na Commentator 254, Sandy alisema kuwa wanaume wanaweza kukosa pesa na bado kuweza kutoa kwa njia kama vile kihisia, kimwili au kiroho.

SANDY KAHUSH
SANDY KAHUSH
Image: INSTAGRAM

TikToker Sandra Kahumba almaarufu Sandy Kahush anasema kuwa hajali kumsaidia mpenzi wake kwa kulipa bili.

Katika mahojiano na Commentator 254, Sandy alisema kuwa wanaume wanaweza kukosa pesa na bado kuweza kutoa kwa njia kama vile kihisia, kimwili au kiroho.

Pia alisema kuwa hataki pesa za mwanamume kwani yeye anajitengenezea na kuwa anaweza kumfanyia mwanamume wake chochote anapokuwa katika nafasi ya kumfanyia kitu.

Sandra hapendi wanaume ambao wanajigamba sababu wana pesa.

“Sitaki pesa yako nitatengeneza yangu, ama naweza kupa. Kama wewe ni mwanamume wangu, nitakufanyia kila kitu.Kama niko nayo nitakupea hata naweza kununulia hiyo gari kama niko nayo,”

Alipoulizwa kuhusu kumsaidia mpenzi wake kulipa bili, alisema kuwa hajali kumsaidia mpenzi wake kwa kulipa bili.

Nawezafanya hivo...Najua watu husema si 50/50 lakini pia inaweza kuwa 80/20, 70/30...Sio lazima kwa mwanamume kutoa 100% kifedha kwa sababu pia wanaweza toa kihisia, kimwili na kiroho,"

"Naweza kukuweka kama uko na future...nakuweka nikiona una bidii, nikiona una future," Sandy aliongeza.

Sandy amepata umaarufu miongoni mwa wanaume kwa jinsi anavyowaongelesha kwa kuwajulia hali.