“Nitaoa wake watatu nikianza kuoa kuanzia mwaka ujao” – MP Peter Salasya

“Pia wanawake wa kukumbatia mitala kama mimi nitaoa wake watatu nikianza kuoa kuanzia mwaka ujao,” alisema Salasya.

Muhtasari

• “Pia wanawake wa kukumbatia mitala kama mimi nitaoa wake watatu nikianza kuoa kuanzia mwaka ujao,” alisema Salasya.

PETER SALASYA
PETER SALASYA
Image: INSTAGRAM

Mbunge wa Mumias Mashariki, Peter Salasya ametangaza rasmi kwamba ataanza safari ya kujukumika kama mume katika ndoa kuanzia mwaka ujao.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Salasya alisema kwamba ataanza kuoa mwaka kesho, lakini akaweka wazi kwamba hayuko tayari kutulia na mwanamke mmoja bali atafululiza hadi 3.

Alitoa wito kwa wanawake kukumbatia ndoa za wanawake wengi kwa mwanamume mmoja, akisema kwamba huko ndiko dunia inakoelekea kwani watoto wa kike wanaozaliwa ni wengi kuliko wa kiume.

“Pia wanawake wa kukumbatia mitala kama mimi nitaoa wake watatu nikianza kuoa kuanzia mwaka ujao,” alisema Salasya.

Mbunge huyo mcheshi amekuwa akimfukuzia mwanasosholaiti Huddah Monroe katika siku za hivi karibuni.

Salasya alisema kwamba alikuwa tayari kumkaribisha Huddah Nchini na hata kufanya mazungumzo na yeye jinsi ya kuanzisha familia, lakini kwa tamko lake hilo, huenda ameahirisha mipango yake ya kumuoa Huddah kwa sasa hadi mwaka kesho.

Swali ni je, Huddah atakuwa mmoja wa wanawake 3 watakaoolewa na Salasya au la, na je atakubali kuwa na wanawake wenza kwenye ndoa moja?