Felicity atangaza kutafuta nyumba ya kuhamia wiki 2 baada ya kuachana na Thee Pluto

"Maeneo ambayo ningependa kuishi sijajua sana lakini singependa kuishi maeneo ya Thika Road. Ningependa kuishi maeneo ya karibu na Town ama maeneo ya Kiambu,” aliongeza.

Muhtasari

• Kuhusu idadi ya watu ambao watakuwa wanaishi katika nyumba hiyo mpya, Felicity Shiru alisema;

‘• Ni mimi, binti yangu Zoey na mlezi na wakati mwingine naweza kuwa na wageni kama dada zangu,"

FELICITY SHIRU
FELICITY SHIRU
Image: HISANI

Mtayarishaji maudhui Felicity Shiru amefichua kwamba yuko katika harakati za kuwinda nyumba ya kuhamia baada ya ndoa yake na Thee Pluto kusambaratika wiki mbili zilizopita.

Katika vlog yenye kichwa ‘Moving Out – House Hunting for a New Home!’, aliyoichapisha mnamo Septemba 23, Felicity alishiriki na mashabiki wake sura mpya anayoanzisha baada ya kuachana na Thee Pluto.

Baby mama huyo wa Pluto alieleza baadhi ya vigezo ambavyo atavizingatia katika nyumba mpya ambayo anatumai kupata hivi karibuni.

“Kama ambavyo mmeona mada ya video hii, ninawinda nyumba na kuna vitu muhimu ambavyo ninaangalia. Ningependa kupata nyumba ambayo iko kivyake, singependelea kuishi kwa apartment. Lakini simaanishi kuna kitu kibaya na nyumba za apartment,” alisema.

‘Ningependa kupata nyumba yenye vyumba 2 au 3 vya kulala. Nahisi kama ninahitaji hiyo nafasi. Maeneo ambayo ningependa kuishi sijajua sana lakini singependa kuishi maeneo ya Thika Road. Ningependa kuishi maeneo ya karibu na Town ama maeneo ya Kiambu,” aliongeza.

Kuhusu idadi ya watu ambao watakuwa wanaishi katika nyumba hiyo mpya, Felicity Shiru alisema;

‘Ni mimi, binti yangu Zoey na mlezi na wakati mwingine naweza kuwa na wageni kama dada zangu, ndio maana nilifikiria pengine nyumba ya nyumba 2 au 3 itakuwa sawa kwa sababu pia nina bajeti maalum kwa ajili ya hiyo.”

Hapo awali, Thee Pluto alikuwa amefichua kwamba Felicity alihama nyumba yao ya ndoa kando ya barabara ya Thika, akiamua kusalia na mamake baada ya kutengana.