Koffi Olomide asisimua Nairobi kwa tamasha la kukata na shoka (+picha)

Koffi Olomide alitokea jukwaani akiwa amevalia suti ya pinki, tisheti nyeupe, kofia nyeupe na buti nyeupe.

Muhtasari

•Koffi Olomide alipiga shoo ya kukata na shoka jijini Nairobi Jumamosi usiku katika uwanja wa maonyesho wa Dome, ASK.

jukwaani
Koffi Olomide jukwaani
Image: RADIO AFRICA EVENTS

Mwimbaji mahiri wa Kongo Koffi Olomide alipiga shoo ya kukata na shoka jijini Nairobi Jumamosi usiku katika uwanja wa maonyesho wa Dome, ASK, kwa hisani ya Radio Africa Events.

Hafla hiyo iliyopewa jina 'Koffi Olomide; The Peace Concert,' lilishuhudia maonyesho kutoka kwa Les Wanyika, Bensoul na Johnny Junior. DJ ken na DJ Twinn 48 walikuwa wacheza santuri wakuu wa usiku huo.

Tamasha lilianza Jumamosi jioni kwa mchanganyiko wa muziki kutoka kwa DJ Ken huku Johnny Junior akipanda jukwaani kabla ya jioni. Les Wanyika kisha wakapanda jukwaani wakiwa wamejipamba na mavazi yote meupe.

Bensoul baadaye alipanda jukwaani naakatumbuiza kwa nyimbo zake maarufu.

Msanii wa usiku huo, Koffi Olomide alitoka akiwa amevalia suti ya pinki, tisheti nyeupe, kofia nyeupe na buti nyeupe.

Wacheza densi wake walivalia nyeupe na nyekundu huku wakipeleka hadhira hadi mwishoni mwa miaka ya 90 hadi 2023.

Tazama picha la tukio nzima:-

jukwaani
Koffi Olomide jukwaani
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS
Image: RADIO AFRICA EVENTS