•Obina alishiriki picha ya skirini ya ujumbe aliopokea kutoka kwa kipusa huyo,ambaye alisema kila mtu ataenda zake ikiwa Obinna angekubali ombi lake la usiku mmoja wa mapenzi.
Mchekeshaji na mwanablogu Oga Obinna ameonekana kushangazwa baada ya shabiki wa kike kumuomba kwa ujasiri kushiriki mapenzi kwa usiku mmoja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Obinna alishiriki picha ya skirini ya ujumbe ambao alipokea kutoka kwa kipusa huyo aliyemuahidi kila mtu ataenda zake ikiwa angekubali ombi lake la usiku mmoja wa mapenzi.
“Obinaaa, One night stand moja tu hivi halafu kila mtu aende zake.” Alisema.
Akijibu ujumbe huo, mchekeshaji huyo alishindwa ikiwa angeufuta, angekubali ombi hilo au kumblock mtumiaji huyo wa instagram.
Hata hivyo alikiri kwamba amependezwa na ujasiri mwanadada huyo alikuwa nao.
“Wheh!!!🤣🤣🤣🤣🤣🤣 napenda kujiamini!!!Mambo, hata hivyo ni matatu…Je, Nakublock, kufuta,kukubali?"
Hatua ya Obinna kutangaza ujumbe huo ilivutia hisia mbalimbali kutoka kwa mashabiki wake wanomfuatilia kwenye ukurasa wa Instagram.
Walitoa maoni tofauti kufuatia ujumbe huo;
Majier49, alisema;
“Huyu dem angekuwa msupa sidhani ungemuanika ivi, jambo lingekuwa moja, kubali,”
Wengine walimshauri akubali ombi la kipusa huyo la kushiriki ngono kwa usiku mmoja
“Mkubali kaka🥵..Perform tu !” Mtumiaji mmoja alisema huku mwingine akisea;,
“Mayoooo,hivi hamskiangi nikiwaambia line ni kubwa,huyu ana overlap,panga line mamaa,huwezi kuja upite tu,”
Jumbe zingine za maoni zilisoma,
“Woiye obi umemwanika mbaya 😂😂😂😂😂😂hata heri angesema anataka kuwa mboch ya kina Lola,”
Awali Obinna alikuwa ameshiriki picha ya skrini ya jumbe nyingine ya kuchekesha aliyopokea kutoka kwa shabiki.
“Obinna nakupenda, mimi tukichumbiana, nakudekeza kama mototo.” Ulisoma.