Mchekeshaji mzaliwa wa Kenya, Elsa Majimbo akiri chuki kwa Wakenya

Wakati alipoulizwa iwapo anawapenda Wakenya, Elsa Majimbo alisema kwa ujasiri "Hapana!"

Muhtasari

•Majimbo , aliwapa changamoto wanamitandao kuonyesha video yake akikiri chuki yake kwa Kenya na kuahidi zawadi ya $1000 (Ksh152,950) kwa yeyote atakayeitoa.

•Wakati akiendelea kujibizana na wanamtandao chini ya chapisho hilo, hata hivyo alikiri kwamba hapendi Wakenya.

Image: INSTAGRAM// ELSA MAJIMBO

Siku ya Ijumaa, mchekeshaji  mzaliwa wa Kenya anayeishi Marekani na Afrika Kusini, Elsa Majimbo alitoa changamoto kwa wanamtandao kutoa video yake akisema anachukia Kenya.

Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na madai kwamba mrembo huyo mwenye umri wa miaka 22 aliikana Kenya na kukiri kutoipenda nchi ambayo alizaliwa.

Hata hivyo, katika kile kilichoonekana kana kwamba anakanusha madai hayo, aliwapa changamoto watumiaji wa mitandao kuonyesha video yake akikiri chuki yake kwa Kenya na kuahidi zawadi ya $1000 (Ksh152,950) kwa yeyote atakayeitoa..

"Nitalipa $1000 kwa yeyote ambaye anaweza kutoa video yangu nikisema maneno 'Nachukia Kenya'," Elsa Majimbo aliandika kwenye Twitter.

Alipoulizwa kwa nini alitoa changamoto hiyo, alikariri kuwa watu wanadai haipendi Kenya ilhali yeye mwenyewe hajawahi kusema hivyo.

"Kila mtu anasema nachukia Kenya wakati sichukii na sijawahi kusema maneno hayo na sitawahi," alisema.

Wakati akiendelea kujibizana na wanamtandao chini ya chapisho hilo, hata hivyo alikiri kwamba hapendi Wakenya.

"Je, unawapenda Wakenya?" Dk.EW. Alimuuliza Majimbo.

Akajibu, “Hapana.”

Mtumiaji mwingine wa Twitter alijaribu kumkaribisha tena Kenya, “Binti mpotevu. Karibu tena."

Akajibu, “Hapana, asante. Toa video tu.”

Hivi majuzi, mchekeshaji huyo alidai kuwa Kenya ina ubaguzi wa rangi  nyeusi (colorism), jambo ambalo lilimfanya kuondoka nchini alipokuwa na umri wa miaka 19.

Colorism ni ubaguzi dhidi ya watu wenye ngozi nyeusi, kwa kawaida miongoni mwa watu wa kabila au rangi moja.

"Nilipokuwa na umri wa miaka 19, nilihama Kenya kwa sababu kulikuwa na ubaguzi wa rangi nyeusi. Nilikabiliana na mengi nilipovuma na hata kabla ya hapo kulikuwa na maoni mengi juu ya 'oh wewe ni giza sana, tazama. hiyo tint, oh yeye ana sura mbaya sana, mbona? Kwa sababu ni mweusi,” Majimbo alisema kupitia Tiktok.

Alisema hakujiona akifaulu nchini Kenya.

"Nilikuwa kama siwezi kamwe maendeleo katika nchi hii na aina hii ya mawazo ... mimi ni mwaminifu kwa kitu kimoja, mfuko. Marekani kila mtu alikuwa anasema, angalia ngozi yako ya kushangaza, inaonekana kama lulu, inang'aa, oh. Kwa nini nisingelipwa kwa dola,” alisema.

Alijiuliza "Je, unaweza kufa kwa ajili ya nchi yako?"

Na akajibu, "Hapana, mimi si mpigania uhuru, mimi sio mwanaharakati."