Mtangazaji Gidi alalamika kuhusu jinsi mahagwe ya rosecoco yalivyoharibiwa jina

“Vijana wameharibu jina la hii maharagwe mpaka ukiiona kwa shelf unaishuku tu,” Gidi alisema.

Muhtasari

•Gidi alibainisha kuwa vijana wa Kenya wamebadilisha maana ya jina ‘rosecoco’ hadi kufikia hatua ambayo imekuwa vigumu sana kuzinunua tena madukani.

•Kwa muda mrefu zaidi, Rosecoco imekuwa ikijulikana tu kuwa aina ya maharagwe yanayouzwa sokoni.

amelalamika kuhusu jinsi maharagwe ya rosecoco yameharibiwa jina
Mtangazaji Gidi Ogidi amelalamika kuhusu jinsi maharagwe ya rosecoco yameharibiwa jina

Mtangazaji wa kipindi cha Gidi na Ghost Asubuhi kwenye Radio Jambo, Gidi Ogidi ameeleza wasiwasi wake kuhusu jinsi jina la maharagwe ya ‘Rosecoco’ lilivyochafuliwa.

Katika taarifa yake siku ya Jumanne, Gidi alibainisha kuwa vijana wa Kenya wamebadilisha maana ya jina ‘rosecoco’ hadi kufikia hatua ambayo imekuwa vigumu sana kuzinunua tena madukani.

“Vijana wameharibu jina la hii maharagwe mpaka ukiiona kwa shelf unaishuku tu,” Gidi alisema kwenye Instagram.

Aliambatanisha ujumbe wake na picha ya kilo moja ya maharagwe ya rosecoco yakiwa yamewekwa kwenye karatasi ya plastiki.

Katika kipindi cha takriban miezi miwili iliyopita, neno rosecoco limekuwa likivuma sana kwenye majukwaa tofauti ya mitandao ya kijamii nchini Kenya.

Kwa muda mrefu zaidi, Rosecoco imekuwa ikijulikana tu kuwa aina ya maharagwe yanayouzwa sokoni.

Lakini katika muda wa miezi miwili iliyopita, Wakenya wamekuwa wakitumia neno ‘Rosecoco’ kurejelea kiungo cha uzazi cha mwanamke.

Yafuatayo ni mambo ambayo hukuyajua kuhusu maharagwe ya Rose Coco:-

  1.  Rosecoco ni maharagwe yanayokaribia kufanana na Red Kidney beans.
  2. Ikilinganishwa na Red Kidney beans, Maharage ya Rosecoco huipa sahani mchuzi wenye rangi zaidi.
  3. Maharage haya ni chanzo kizuri cha protini na yana kiasi kikubwa cha nyuzi lishe.
  4. Wakati wa kupanda, nafasi kati ya mimea inapaswa kuwa 60x60 (cm).
  5.  Maharage ya Rosecoco ni mojawapo ya aina zenye gharama ndogo za uzalishaji.
  6. Maharage haya hayahitaji uangalizi maalum kutoka kwa mkulima mbali na kupanda na kupalilia.
  7.  Aina hii ya maharagwe imekadiriwa kuwa na uwezo wa kustahimili magonjwa na hubadilika vyema kulingana na hali ya hewa ya Kenya.
  8.  Maharage ya rosecoco yanaweza yasistawi katika maeneo yaliyojaa maji na yanaweza kufanya vibaya kwenye udongo wa kichanga.

Maeneo ambayo maharagwe haya ya Rosecoco hustawi nchini Kenya, ni pamoja na:• Eneo la Magharibi

  • Eneo la Kati
  • Eneo la Nyanza
  • Eneo la Mashariki na Baadhi ya maeneo ya eneo la Kaskazini
  • Eneo la bonde la ufa

Kulingana na eneo lako, mfuko wa kilo 90 wa bei ya maharagwe ya Rose coco nchini Kenya huanzia Ksh. 7,000 hadi Ksh. 9,900.

Rosecoco inarekodi bei ya juu zaidi katika soko la Kenya kutokana na mahitaji makubwa.