"Napenda nyoka sana!" Diamond akiri baada ya kujipatia nyoka wa kuweka nyumbani (+video)

Diamond alifichua kuwa nyoka huyo wake anatambuliwa kwa jina Chichi.

Muhtasari

•Staa huyo wa Bongo mwenye umri wa miaka 32 alimtambulisha nyoka huyo wake kama rafiki yake mpya.

•Mwimbaji huyo anayetambuliwa kote duniani alifichua kwamba nyoka huyo wake atatambuliwa kwa jina  Chichi.

Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Bosi wa WCB Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz amejipatia mnyama aina ya nyoka wa kuweka nyumbani.

Katika tangazo lake kwenye Instagram, mwanamuziki huyo alibainisha kuwa siku zote kumiliki nyoka kipenzi imekuwa ndoto yake.

Staa huyo wa Bongo mwenye umri wa miaka 32 alimtambulisha nyoka huyo wake kama rafiki yake mpya.

"Siku zote nimekuwa na shauku ya kuwa na nyoka wangu kama kipenzi ❤️🐍.. jameni kukutaneni na rafiki yangu mpya," alitangaza siku ya Ijumaa.

Aliambatanisha ujumbe huo na video yake akicheza na mnyama huyo anayeteleza huku kundi kubwa la watu wakiwa wamemzunguka.

Katika video hiyo, Diamond alisikika akikiri upendo wake mkubwa kwa nyoka na kueleza furaha yake kwa kumpata wa kufuga nyumbani

"Huyu mimi namfuga mnyama huyu nyumbani. Mimi napenda nyoka sana," alisika akisema.

Umati ulitazama kwa udadisi alipokuwa akichezea na nyoka huyo kwa usaidizi wa mwanamke aliyekuwa akimuonyesha jinsi ya kumshika. Hakuonesha uoga wowote na badala yake alionekana kufurahi sana kumshika.

Mwimbaji huyo anayetambuliwa kote duniani alifichua kwamba nyoka huyo wake atatambuliwa kwa jina  Chichi.

Katika hali ya kawaida nyoka sio wanyama wa kupendwa miongoni mwa watu wengi. Wengi wa wanyama hao wana sumu ambayo inaweza kusababisha kifo au ugonjwa mbaya mara tu wanapomng'ata mtu.

Baadhi ya jamii za Kiafrika huhusisha mnyama huyo na uchawi na hivyo kamwe hawawataki karibu nao. Wale wanaofuga wanyama hao mara nyingi huchukuliwa kuwa wanashiriki katika uchawi.

Tazama video hapa:-