“Sitawahi kuwa sawa tena!" Mwimbaji Nazizi amkumbuka kwa uchungu marehemu mtoto wake

Nazizi Hirji amezungumza kwa hisia kuhusu kifo cha mtoto wake wa miaka mitatu, Jazeel Adam.

Muhtasari

•Nazizi alikiri kwamba haendelei vizuri baada ya kifo cha mwanawe na kushangaa jinsi maisha yatakuwa bila mvulana huyo mdogo ambaye alimthamini sana.

•Alibainisha kuwa marehemu Jazeel alileta furaha kubwa kwa familia na akafichua kuwa nia kuu ya mwanawe ilikuwa ni kwamba wote wawe pamoja.

amemkumbuka kihisia mwanawe
Nazizi amemkumbuka kihisia mwanawe
Image: INSTAGRAM// JAZEEL ADAM

Msanii mkongwe wa dancehall na rap wa Kenya, Nazizi Hirji amezungumza kwa hisia kuhusu kifo cha mtoto wake wa miaka mitatu, Jazeel Adam.

Jazel alifariki kufuatia ajali iliyotokea Desemba 25, 2023 katika hoteli moja nchini Tanzania ambako Nazizi na familia yake walikuwa wakiishi. Mwili wa mvulana huyo baadaye ulisafirishwa hadi Kenya baadaye ambako alizikwa mnamo Desemba 26, 2023.

Katika taarifa iliyojaa hisia kali kwenye ukurasa wake wa Instagram, mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la Neccesary Noize alikiri kwamba haendelei vizuri baada ya kifo cha mwanawe na kushangaa jinsi maisha yake yatakuwa bila mvulana huyo mdogo ambaye alimthamini sana.

"Nimevunjika, nimezama gizani, sitakuwa sawa tena. Je, nitaendeleaje bila nuru ya maisha yangu? Kwa nini niamke kila asubuhi, ili tu kulia na kuku’miss siku nzima? Ulitupenda sana, na tulikupenda hata zaidi, jazzy wangu wa thamani,” Nazizi aliomboleza Jumapili jioni.

Mwimbaji huyo mzaliwa wa pwani aliambatanisha taarifa yake na video inayoonyesha kumbukumbu nzuri ambayo familia ilishiriki na marehemu Jazeel.

Alibainisha kuwa marehemu Jazeel alileta furaha kubwa kwa familia na akafichua kuwa nia kuu ya mwanawe ilikuwa ni kwamba wote wawe pamoja.

"Video hii inanasa roho yako katika sekunde chache. Ulichowahi kuhitaji ni sisi 4 kuwa pamoja kila wakati. Ulileta maana mpya kwa familia,” aliandika.

Nazizi aliendelea kuzungumzia jinsi maisha yamekuwa katika takriban siku hamsini zilizopita tangu mtoto huyo wake wa miaka mitatu kupoteza maisha kwa bahati mbaya.

“Kijana wangu, maisha hayavumiliki bila wewe 💔💔. Mama anakupenda sana, na ningefanya chochote ili kuwa nawe tena. Sitawahi kuwa sawa, ulimwengu wangu ulisimama uliponiacha jiji. I miss you my sweet boy special,” Nazizi alisema.

Mamia ya watumiaji wa mtandao ikiwa ni pamoja na Wakenya maarufu walikusanyika chini ya chapisho la Nazizi kumfariji na kumtia moyo kufuatia kupoteza kwake.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya;-

Anerlisa Muigai: Ohhh 😢, so sad we had to connect during this difficult time. Know I am here for you. Only those who have lost a loved one understand each other. I have your back no matter what. Endless hugs. Rest In Power Sweet Jazy.

Talia Oyando: Oh Jazy you are love and you are loved. We walk this journey together Naz. Love you.

Zuena Kirema: May Allah grant you the strength to overcome this pain,stay strong my dear.

Vanessa Mdee: Sis. I’m so sorry. Sina cha kusema. Ila MUNGU ALIYE HAI awape nguvu na faraja 🙏🏽🌹

Femi One: We love you Naz 😤. I’m so sorry praying for you.