Wakenya washangazwa na ukuaji kasi, kiingereza na ukaidi wa bintiye Karen Nyamu wa mwaka mmoja (+video)

Karen Nyamu ambaye alionekana kushtushwa alihofia kwamba bintiye wa mwaka wake mmoja tayari amejifunza kuwa mkaidi.

Muhtasari

•Nyamu alionekana akizozana kidogo na bintiye kuhusu bangili tatu ambazo msichana huyo wa umri wa mwaka mmoja alikuwa amevaa.

•Licha ya agizo la kutovaa bangili za mikononi, Nimmo alimwambia mama yake kwa dharau, “Naweza kuvaa!” na kuendelea kucheza

Karen Nyamu, Taraya Wairimu na Samidoh
Image: HISANI

Siku ya Jumatano asubuhi, seneta wa kuteuliwa Karen Nyamu alionyesha klipu fupi ya video iliyomuonyesha akitangamana na mtoto wake mdogo.

Taraya Wairimu almaarufu Nimmo ni mtoto wa pili wa mwanasiasa huyo na mpenzi wake Samuel Muchoki almaarufu Samidoh aliyezaliwa Februari mwaka jana.

Katika video hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, Bi Nyamu alionekana akizozana kidogo na bintiye kuhusu bangili tatu za mkononi ambazo msichana huyo wa umri wa mwaka mmoja alikuwa amevaa.

“Good morning, good night, good morning,” alisikika Nimmo akisema katika hali ya furaha kabla ya mama yake kumkatisha akitaka kujua ni nani aliyempa bangili hizo.

"Ni nani aliyekupa hii, na hii mikononi mwako? Je, ni Teana alikupa hii? Alikutengenezea wewe? Hapana, huwezi kuvaa hizo, zinaonekana tatanishi mamaa,” Karen Nyamu alimwambia bintiye huku akikagua mikanda aliyovaa mikononi mwake.

Licha ya agizo la kutovaa bangili za mikononi, Nimmo alimwambia mama yake kwa dharau, “I can wear!” na kuendelea kucheza kitandani.

Katika chapisho lake la Facebook, Karen Nyamu ambaye alionekana kushtushwa alisema kwamba bintiye wa mwaka wake mmoja tayari amejifunza kuwa mkaidi na akashangaa nini kingefuata.

“Haka hakatambui sheria, kameshajua ni ukaidi. Tushoke turore naku?? (Alafu tuangalie wapi sasa),” Bi Nyamu aliandika.

Wanamtandao waliopata kuona video hiyo walifurahishwa na ukuaji mkubwa wa mtoto huyo wa tatu wa seneta huyo na ukweli kwamba anaweza kuzungumza Kiingereza.

Angalia maoni ya baadhi ya watumiaji wa Facebook;

Eva Waihuini Ngacha: Mdoli mzuri, anaweza weeaaa

Stycie Waweru: Yeye ni mrembo na mwerevu

Mbote Njogu: Ni kakubwa sasa ongeza kengine.. kashajua kuongea kizungu

Grace Omuya: Mrembo sana, katika umri huo sikujua hata kutaja jina langu.

Precious Joy: Huyu ni wajanja wacha tu