KURIA: Mwili wa mwanafunzi wapatikana msituni

Picha kwa hisani ya: commercialpressuresonland.org

Mwili wa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo umepatikana katika msitu wa Tagare kilomita moja kutoka nyumbani kwao.

Kwa mujibu wa OCPD wa Kuria magharibi Paul Kiogora, mwili wa mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu David Machage ulipatikana baada yake kutoweka kwa muda wa siku tatu.

Kiogora aliongeza kuwa mwili huo ulikuwa na majeraha ya kifaa kibutu na pia kulikuwa na damu katika eneo hilo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Machage ukisubiri kufanyiwa upasuaji.