KUMBUKUMBU: Tazama Mbusii Akimfunza Kidosho Huddah Kucheza Densi

huddah
huddah
Zaidi ya miezi mitano iliyopita katika kipindi nambari moja nchini kwanzia mida ya saa tisa alasiri hadi saa moja jioni, cha Mbusii na Lion Teketeke watangazaji maahiri Mbusii na Lion deh, waliwashangaza huku wakiwafurahisha wengi baada ya kumfunza kidosho Huddah Monroe jinsi ya kusakata densi katika mtindo wa Reggae.

Watangazaji hao wana kitengo cha 'Gyal Dem Wednesday' kila siku ya Jumatano ambapo husherehekea wanadada na kina mama wote nchini, haswa wapenzi wa muziki wa reggae.

Siku hiyo mmoja wa vidosho warembo zaidi nchini, Huddah Monroe aliyevuma kwa mitindo yake ya mavazi, na urembo wake wa kufana, aliweza kualikwa studio.

Alipokubali mwaliko wa Mbusii katika studio za Radio Jambo, Kidosho Huddah hakusita kwa kuonesha umaahiri wake wa kusakata muziki wa reggae huku akiwaacha Mbusii na Dj Dickie vinywa wazi.

Isitoshe, Mbusii naye alichukua fursa hiyo kumfunza kidosho huyo jinsi ya kusakata densi kama mwana reggae halisi.

Tazama kanda ifuatayo.