PATANISHO: "Hata Akifa Mazishi Yake Nisialikwe Na Mazishi Yangu Asiitwe"

steve
steve
Jameni mizozo kati ya ndugu wawili ilifikia wapi kiwango cha watoto wa tumbo moja kuchukiana na kuamua kuendeleza chuki hadi kaburini?

Haya yalishuhudiwa hapo jana katika kitengo cha Patanisho ambapo ndugu wawili, Purity na bwana Kim waliwashangaza wengi waliposhindwa kupatana huku wakiwa na misimamo mikali dhidi ya familia yao na wazazi wao wenyewe, huku mmoja akitaka amani katika familia mwingine hajalishwi kamwe.

Kizazaa kilianza wakti Purity alipo omba apatanishwe na nduguye mkuu Bwana Kim, kwani kwa boma lao wakiwa wadogo walikuwa na shida tele, mojawapo ikiwa mama yao kuwa na tabia ya kupigana na babayao.

Purity aliongeza na kusema kwa ajili ya yale, chuki iliingia kwa watoto na baba yao akaoa mke mwingine.

"Juzi ndugu zangu walipigana wakisema watoto wao hawafai kuingia kwa boma za wengine. Kila mtu ako kivyake hakuna umoja katika boma letu na naomba tupatane na ndugu yangu ili pamoja tulete kila mtu pamoja na tupendane." Alijieleza Purity.

"Mimi niko sawa nimekuwa nikishughulikia mama yetu kwa hivyo kivyangu sina shida yoyote na mama yangu kwa hivyo hayo maneno yamenishangaza sana. Hata akifa mazishi yake nisialikwe na mazishi yangu asiitwe." Aliwashangaza wengi bwana Kim huku akigadhabishwa na hatua ya Purity kukiri kuwa hawana umoja katika familia yao.

"Basi hata ukifa sitakuja lakini naomba tuwe pamoja hayo tu." Aliongeza Purity ikiwa ishara tosha wawili hawa wana tofauti kubwa zaidi kabla ya bwana Kim kukata mawasiliano.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be