PATANISHO: Bwanangu Kazi Yake Ni Ku Bet Na Halipi Karo Wala Kununua Chakula

Jackline 32, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe Charles 40, akidai "Naomba akujie bag yake tafadhali kwa sababu nimeskia nimechoka na yeye."

"Hakuna kitu imefanyika lakini naona jamaa hayuko supportive, mimi naona akiona ni ngumu sana kama yeye ni bwanangu au la aniambie kwani amekuwa akipotea potea.

Mimi ni bibi wa pili najua ana mke hiyo yote sikatai lakini akielekea kule huwa ananisahau kwani hana shughuli ya watoto, hapigi simu watoto hashughulikii. Akirudi hataki kujua mnaendeleaje kwani hukaa siku mbili pekee na kwa yule mwingine huishi wiki mzima." Alisema Jackline akiongeza kuwa mke wa kwanza hawaongei kamwe kwani hakufurahia kuwa aliingia kwa ile ndoa ambayo ameishi kwa miaka saba.

"Watoto wake walikuwa wananitembelea lakini ilifika wakati fulani wakachapwa baada ya kunitembelea na tangia hapo sijawahi waona tena." Alisema Jackline.

Alipopigiwa simu bwana Charles alidai kuwa ni kweli wameoana na hakuna kile alichoficha bi Jackline akiongeza kuwa "Shida aliyo nayo ni ugomvi kila mara. Juzi kuna mahali nafanya kazi na nikawa na shida fulani ya kifedha kidogo kidogo wale watu wakanishtaki kwa polisi na nikawekwa jela usiku mzima na hata Jackline hakuja kuniona. Nilipotoka nikampata hayuko na aliporudi aliniadikia ujumbe kwa simu akisema kuwa hataki kuniona kwa nyumba yake."

Jackline naye alijitetea akisema kuwa imekuwa mtindo wake kufungwa na alikuwa amechoka. Isitoshe mumewe alikuwa na tabia ya kutuma mtoto dukani na jina lake akidai kuwa ni yeye ametuma. "Akifika kwa nyumba kazi yake ni ku bet na halipi karo wala kutununulia chakula jameni."

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be