PATANISHO: Bangi Mke Wangu Alijua Navuta Na Pia Mamake Alijua

patanisho
patanisho
Siku moja tu baada ya jamaa kukiri kuwa angetoa uhai wa mpenziwe, kisa na maana kutemwa, jamaa kwa jina Freddy alituma ujumbe akiomba apatanishwe kwani ana mipango ya kumuua shemeji yake kwani ndiye aliyechochea mkewe kuondoka nyumbani.

Freddy aliomba apatanishwe na mkewe, Levina akidai kuwa siku moja alipo ondoka kuelekea kazini, dadake Levina alimchukua na kumpeleka nyumbani, huku akidai "Sasa nafikiria kumtendea unyama."

"Mke wangu tumeishi na yeye, saa hizi tunaelekea miaka mitano kwani tulipatana baada ya kumaliza chuo na tukabarikiwa na watoto wawili. Sikatai kuwa nimekuwa na makosa kidogo kidogo ya kumpiga makofi makofi lakini yote tulisuluhisha.

Juzi nilisafiri hadi mariakani kazini na mke wangu akanipigia simu akisema kuwa ametoka nyumbani na ameelekea na watoto. Sasa huyu dadake nashuku ndiye aliyemshawishi aondoke nyumbani lakini naelezwa kuwa sasa hivi amerudi Nairobi lakini sijui aliko." Alieleza bwana Freddy.

Alipopigiwa simu, Bi Levina alisema kuwa yuko Nairobi na kuwa anaishi na mamake mzazi.

"Huyu mtu huwa mtu wa kuvuta bangi kwanza kitu kidogo yeye hunipiga na hataki kuskia kwani chochote atakacho hataki nipinge. Siku moja nikiwa Nairobi, jamaa fulani alinisalimu na kumbe sikujua kuwa ilimuudhi, jamaa huyo akanisalimu na lugha ya kijaluo kufika nyumbani mida ya saa nne mume wangu akanitandika bila sababu." Alijieleza bi Levina.

"Nimeamua kuishi pekee yangu kwani kuna mda alimtusi mamangu mzazi." Aliongeza.

"Nilikuwa nafanya kazi ngumu ya juakali na hapo ingebidi nivute bangi lakini katika kazi mpya imebidi nibadilishe tabia." Alijitetea bwana Freddy.

"Nilikuwa nimepiga simu ili nikuombe msamaha lakini inakaa nikama mapenzi imeisha kwa hivyo rudisha mtoto wangu wa kiume wewe ubaki na wa kike. Bangi alijua navuta hata mamake anajua navuta." Aliongeza huku akiwa mwingi wa hasira.

"Huyu jamaa ana vitisho chungu nzima kila saa anasema kuwa ataua watoto pia na familia yangu, mimi sitaki maneno yake na watoto hatapata pia." Alisema Levina.

Pata uhondo kamili

&feature=youtu.be