PATANISHO: Kazi Ya Bodaboda Hunipa Majaribu Ya Mipango Ya Kando

Philemon kutoka Webuye alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mkewe Irene.

Kulingana na Philemon mkewe aliondoka tarehe 15/7/2016 baada yake kumpa pesa za kuhudhuria matanga na aliporudi kutoka kazini, mkewe hakuwa. Isitoshe alipompigia simu alisikia yuko Nakuru na tangia siku hiyo hajawahi rudi.

"Kila siku nikifuatilia husema atarudi lakini hadi wa leo hajawahi rudi. Watu walimueleza kuwa nina mipango ya kando. Ni ukweli nina mipango ya kando lakini huwa nazungumza na watu wengi katika biashara yangu ya bodaboda lakini sasa hivi nimewacha." Alieleza Philemon ambaye pamoja na mkewe wamekuwa pamoja kwa mda wa miaka minne, huku wakijaliwa watoto wawili.

"Mwaka uliopita mwezi wa kumi na moja nilimtumia fedha za usafiri lakini hakuja na hapo akasema kuwa nisimtumie fedha kwani atajileta mwenyewe akipata nauli na tangia siku hiyo hajawahi kuja." Aliongeza huku akifichua mbinu zenye wana bodaboda hutumia kupata wanadada pia na majaribu wanayokumbana nayo.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be