PATANISHO: Nasikitika Kumchoma Dadangu Usoni Kwa Chai Moto

Bi Margret alituma ujumbe akiomba na dadake bi Mary ambaye walipigana vibaya sana na akamchoma.

"Tulikuwa tumeelekea mahali bash na dadangu na tulikuwa walevi sote, sasa wakati tulitaka kuondoka akawa amenizuia kwani nilitaka niende kwani asubuhi yake nilikuwa nafungua duka.

Sasa kupanda pikipiki dadangu akanivuta akaniangusha akaanza vita akidai kuwa hakuna jinsi ningeenda nyumbani na tulifika na yeye.

Sasa asubuhi kurudi kwa nyumba nilienda kutayarisha chai na nilikuwa na hasira kuu. Hapo nikamwagilia chai moto na akalazwa hospitalini. Tulizungumza naye akiwa hospitalini na nikamueleza nimemsamehe lakini sahii hatuzungumzi kwani hata simu zangu hajibu." Alijieleza Margaret.

Alipopigiwa simu bi Mary alieleza kuwa "Sikutaka aende nyumbani, sasa kufika nyumbani sijui ni hasira gani zilitokea kwani hata yeye mwenyewe alijutia sana na akanipigia simu.

Mimi nia yangu ilikuwa kumzuia asifanye kitu kibaya na sijui nini kilitokea, kwani aliniitisha kila kitu kama majani na sukari aweke kwa sufuria sasa akachukua yale maji akanirushia na akatoroka kwenda kwa polisi."

Wanadada hao wawili walikuwa wangwana sana na walizungumza na kutatua hayo yote.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be