Mtahiniwa Alazimika Kuufanya Mtihani Wa KCSE Hospitalini Baada Ya Kujifungua

Mwanafunzi mmoja wa shule ya upili ya Lutacho eneo bunge la Webuye Mashariki kaunti ya Bungoma alilazimika kuufanyia mtihani wake katika hospitali ya Kimisheni ya St. Bakhita Misikhu baada ya kujifungua usiku wa kuamkia jana.

Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo Stephen Korir alidokeza kuwa Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyejifungua usiku wa kuamkia jana yuko katika hali nzuri na kuwa ataruhusiwa kuondoka wakti wowote.

Naye mamake mwanafunzi huyo Bilha Nangila alielezea furaha yake ya kupata mjukuu na kuongezea kuwa yuko tayari kumlinda mjukuu wake ili kumpa bintiye wakti mwafaka wa kukamilisha mtihani wake.

-Brian Ojamaa