PATANISHO: Mimi Siwezi Ishi Kwa Miti Kama Ndege Kwa Sababu Ya Babako

Bridget kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe Gabriel ambaye kabla wameona kwa miaka tisa.
"Mume wangu alikuwa ananichukua ni kama mimi sio bibi yake na kwa nyumba pia hatukuwa tunaelewana. Mara kadhaa alikuwa anarudi nyumbani akiwa amechelewa na kila nikimuuliza alipokuwa ananikasirikia na hapo hatukuwa tunaelewana." Alieleza.

"Mimi siwezi ishi kwa miti kama ndege kwa sababu ya babako. Kama mimi ndio nina shida kwa ndoa wewe enda tu na usirudi." Alisema bwana Gabriel huku akiwa na wingi wa machungu.

Huwezi toroka kwangu nikiwa kazini kisha nianze kusumbuliwa na babako huku nikiteseka na watoto. Isitoshe ulikuwa Kitale na jamaa mwingine." Aliongeza akidai kuwa baada ya mkewe kutoweka ameshatafuta mke mwingine na mipango ya kumleta nyumbani inaendelea.

Licha ya maneno makali wawili hao hatimaye walirudiana.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be