PATANISHO: Bwanangu Alichukua Simu Yangu Na Kumpa Mpango Wa Kando

Mama Chantelle akiomba apatanishwe na baba Chantelle.

"Hapo nyuma tulikuwa tunakosana na mume wangu kwani alikuwa anatoka nyumbani, anarudi saa sita ya usiku na nikimuuliza ananichapa na nina mtoto mdogo wa mwaka mmoja unusu.

Kuna mwanadada mmoja ambaye alikuwa anampigia saa sita za usiku, anajifunga taulo na kwenda kuongelea nje ya nyumba. Nikimuuliza ananipa na nikimuuliza hiyo ni vita. Alikuwa ananitandika na kunitolea vitu vyangu nje ya nyumba huku akidai yule mwanadada ana haki ya kumpigia simu.

Kitu kingine watu wao hawanipendi hata, isitoshe simu ambaye alikuwa ameninunulia alimpelekea yule mwanadada. " alijua Mama Chantelle ambaye aliongeza kuwa bwanake hakuwa anashughulikia familia yake.

Kumpigia simu siku fulani akanieleza kuwa ameoa mke mwingine baada ya kuondoka kwake jambo ambalo lilisisitizwa na watu wake wakidai kuwa nijipange." Aliongeza.

Juhudi za kumpata Baba Chantelle hazikufua dafu.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be