Nimekuwa nikiletea mume wangu wanawake nyumbani

Cynthia kutoka Kawangware alimshangaza mtangazaji Annitah Raey aliposimulia jinsi yeye alikuwa na tabia ya kutongoza wanawake kwa niaba ya bwanake na kuwaleta kwa nyumba.

Kulingana na mwanamke huyo, bwanake alikuwa na tabia za mipango ya kando na kwa kuwa hakuwahi ona kiini cha kumpigania, ilikuw inamlazimu kuwaleta wanawake ambao alikuwa anawatongoza kwake nyumbani ili aelewe chenye kilimpendeza bwanake.

"I am 36-years of age, 12 years in marriage. Mimi pia mimi nimeolea mume wangu bibi na nikamleta kwa nyumba. Miaka miwili ndani ya ndoa nilikuwa naishi vizuri na nikapata mtoto wa kwanza. Kidogo kidogo mpango wake wa kando akaanza matusi na maneno ya mipango ya kando." Alisimulia Cynthia.

Nikambembeleza nikamwambia pia wewe ni mwanamke kama mimi na ulitongozwa kama mimi. Bwana kutoka kazini akapata mwanamke nyumbani na tukaishi pamoja, maanake si anampenda na anamtaka? Wacha basi nione uzuri wa huyu mwanamke nijifunze naye.

Aliongeza,

waliishi pamoja kwa miaka miwili na akachoka naye akaanza kumchapa kwa nyumba na wakafukuzana. Tena vile vile akapata mwingine, Annitah mimi huwa siongei akifanya jambo mimi humuangalia tu.

Alisema kuwa juhudi hizo zote zilimsaidia kupigania furaha yake kwani sasa amenenepa na yuaishi maisha mazuri pamoja na watoto wake.

Sasa sikuhizi huniangalia tu hivi, sahizi ukiniona nimenenepa, stress sina , house girl nimepata na wananifanyia kila kitu. Hiyo isitishe wanawake wacha wapate house girls wenyewe watajitoa tu.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be