Wanafunzi ndio wanaochangia idadi kubwa ya wasichana wanaojifungua Webuye

Imebainika kuwa idadi kubwa ya kina dada wengi wanaojifungua katika eneo bunge la Webuye magharibi ni wasichana wa shule walio kati ya umri wa miaka kumi hadi miaka kumi na tisa.

Haya ni kwa mujibu wa kaimu afisa wa matibabu wilaya ya webuye magharibi, Alfred Nyongesa Eure, anayesema kuwa hospitali nyingi eneo hilo zimeandikisha idadi kubwa ya wasichana hao na kuwataka washika dau mbalimbali kusaidia kuhamasisha wasichana wadogo kuhusiana na ngono ya mapema.

Kauli hiyo imetiliwa mkazo na kaimu mshirikishi wa serikali ya kaunti ya Bungoma katika eneo bunge la Webuye magharibi Eunice Simuli anayesema kuwa wazazi wengi wamefeli katika majukumu yao na kuchangia katika utovu wa nidhamu kwa wanao.

-Brian Ojamaa