Mcheshi Fred Omondi afichua ukweli wa mwendazake ndugu yake Joseph

Mchekeshaji Fred Omondi ijumaa alisema kuwa mwendazake ngugu yake Joseph alisema uongo kuwa aliacha kutumia vibaya dawa za kulevya.
"Kuna wakati tulimpata akitumia dawa za kulevya ilinibidi nimlete kwangu na alikaa kwa muda ,"Fred alieleza Ijumaa.

Familia iliweza kumuunga mkono na kulipiwa kodi ya  nyumba kisha akapewa pesa ili aweze kujikimu kimaisha,wakifikiri kuwa atabadilika.

Lakini walisahau kuwa mtu ambaye amezoea kufanya kitu hawezi kuwacha kwa haraka kwa maana kitu hicho kinakua kimeshaa muathiri tayari na kumuingia kwa roho lazima akifanye na hawezi kukaa bila kukifanya.

"Kisha tuliweza kuamua kumsaidia ndugu yangu,nafikiria hapo ndipo tulikosea na kumharibu kwa sababu alitushawishi kuwa amebadilika na anaendelea mzuri,"Alizungumza Omondi.

Fred alitangaza kuwa ndugu yake Joseph alifariki mwaka jana baada ya kupigana vita kwa muda na dawa za kulevya.

Mcheshi huyo alisema kuwa ndugu yake alikuwa ameathiriwa sana,"Ilikuwa jambo ngumu sana kwa maana tulig'ag'ana na yeye miaka na miaka.

"Alig'ag'ana na ulevi,na tuliharibu wakati wetu mwingi tukimtafuta badala ya kukuwa pamoja,"Fred alisema.

Fred Omondi aliweza kumtafuta kwa zaidi ya miaka miwili wakati alipompata kwa bahati mbaya aliweza kuaga dunia kwa maana alikuwa katika hali maututi.

Hata hivyo waliweza kupitia hayo yote lakini sasa wananguvu na wamezika hayo yote katika kaburi ya sahau.

Fred anajulikana kama kufanya uchekeshaji katika vipindi tofauti ikiwemo 'churchchill'.Hayo yote yalianza enzi zile alipokuwa akikua.

"Siezi na sitawahi fanya biashara na maisha yangu ya utotoni kwa kitu chochote wala lolote.Nilikuwa na kaka yangu ambaye alikuwa mcheshi pia babayangu alikuwa kibonzo zaidi,"Fred aliongea.

Kwa bahati mbaya waliweza kuwa poteza wazazi wao bado wakiwa wachanga.

"Wakati wazazi wetu walipoaga dunia tuliweza kuwa na wakati mgumu,kwa sababu ilimlazimu ndugu yangu afanye kazi akiwa shule ya upili

"Mimi ni kitinda mimba na alikuwa anilinde na ajikimu pia anikimu kimaisha,"Alisema Fred.

Yote tisa kumi ni kuwa kwa sasa Fred anafanya mradi wa kipindi katika runinga, mradi unaoitwa'Black and White',itakayokuwa inaonyeshwa katika runinga.