Mume wa mtetezi wa haki aliyepotea Dandora ahofia maisha yake

Wazazi wa Carolyne Mwatha
Wazazi wa Carolyne Mwatha
Mume wa mtetezi wa haki wa Dandora aliyepotea ambaye alikuwa anahusika na kesi ya mauaji yasiyo na haki jana alisema kuwa anahofia maisha yake yanaweza kuwa hatarini.

Alisema kuwa anahofia kuwa yeye ndiye anaweza kuwa lengo ambalo linafuatia, mke wake Carolyne Mwatha aliripotiwa kupotea Alhamisi wiki iliyopita.

Mume wake Joshua Ochieng mwanabiashara katika nchi ya Dubai alisema kuwa kupotea kwa mke wake kulimueka hofu kwa maisha yake pia na watoto wake.

Maandamano yatafanyika hivi leo kwa kuchunguzwa na haki ya haraka. Ochieng alisema kuwa alitoka Dubai Jumapili ili kuja kumtafuta mke wake.

Mwatha alikuwa meneja mkuu na pia mwanachama mwanzilishi wa (Dandora Community Justice center), ni kikundi cha kuwatetea haki za wananchi ambacho uhifadhi mauaji yasiyo ya haki na ukatili wa polisi.

Ochieng aliweza kuwasiliana na mke wake kupitia mtandao wa kijamii wa Whats App Jumatano.

"Tulikuwa tunaongea na mke wangu karibu usiku mzima jumatano, asubuhi aliweza kunitumia ujumbe ya salamu za asubuhi, kwa sababu ya kutofautiana kwa masaa niliweza kujibu nikiwa nimechelewa," Alizungumza Joshua.

Alisema kuwa aliweza kumpigia Mwatha simu mara mbili na mtu kupokea ilhali hakuongea.

"Nilimpigia simu mara nyingi nilipoamka ilhali hakuwa ana chukua simu, nilifikiria ni kawaida kwa maana ilikuwa ni siku ya kazi, nilidhani kuwa ako katika mikutano," Alieleza Ochieng.

Ochieng aliingiwa na wasiwasi wakati mke wake alikosa kumpigia tena kisha akawapigia wenzake ndipo waliweza kumuambia kuwa Mwatha hajaenda kazi siku hiyo.

"Sina hakika kuwa msichana wangu yuko mahali sawa ama ana usalama," Ochieng alisema.

Hii ni baada ya mfanyakazi wa nation media kupotea na kupatikana akiwa amefariki katika chumba cha kuifadhi maiti. Polisi walisema kuwa wataakikisha wamepata namba ya mwisho ambayo ilimpigia Mwatha ilikujua kilicho sababisha apotee.

"Hatuwezi tawala kitu chochote, kazi amabayo tunafanya ni hatari, na tuliweza kupokea vitisho kama watetezi wa haki," Alinena Olal.

Alisema kuwa Mwatha alikuwa na faili ya kesi ya polisi waliowapiga watu sita risasi katika eneo hilo la Dandora mwaka jana.

Wenzake Mwatha waliweza kusema kuwa mwenzao Mwatha aliwaambia hajihisi vizuri Jumanne na hataripoti kazini lakini jumatano wakakua hawamfikii kwa njia ya simu kwa maana ilikuwa imezimwa.

"Kufikia sasa tuna wasiwasi kwa mana Caro si rafiki ambaye huwa haongei,"Alisema mwenzake Omondi.

Omondi alisema kuwa wamekuwa wakipea wananchi haki zao,

"Tumekuwa tukipa haki ikuwe ni polisi, mwananchina raia," Omondi alizungumza.

Gavana wa Nairobi Mike Sonko ameweza kutoa 300,000 kwa yeyote ambaye anafahamu mwanaharakati huyo aliko, na kusema kuwa kama kuna mtu yeyote aliye na habari kumuhusu aweze kupiga simu katika kituo cha polisi kilicho karibu.