Mpenzi wa Kori, Judy Wangui, na dereva wa texi Mathenge kushtakiwa leo

Mpenzi wa Joseph Kori, Judy Wangui na Michael Mathenge wanatarajiwa kuwasili mbele ya mahakama ya kaunti ya Kiambu kwa kushtakiwa kwa kumuua mwanabiashara Mary ambaye alikuwa ni mke wa Kori.

Kori mume wa mwendazake Mary Wambui aliweza kuachiliwa Alhamisi wiki jana kutoka kituo cha polisi cha Gigiri, hii ni baada ya wachunguzi kushindwa kupeana ushahidi kuwa alihusika na mauaji hayo.

Kori aliweza kukaa rumande kwa muda wa wiki tatu, hakimu mkuu Stella Atambo alikuwa amewapa polisi siku 14 kisha kuwaongezea siku 10 ili waweze kumaliza uchunguzi wao.

Mary aliweza kutoweka Januari 26 kisha kupatikana akiwa ameuawa na kutupwa katika eneo la Juja.

Baada ya uchunguzi kufanyika polisi wa uchunguzi waliweza kuamini kuwa Kori hakuweza kuhusika katika mauaji hayo ya Mary Wambui.

Pia polisi waliweza kuamini Wambui aliweza kufariki baada ya vurugu na kupigana na Wangui huku akitafuta nia na njia zote za kumficha marehemu.

Judy Wangui alikuwa mpenzi wake Kori licha ya Kori kuwa na familia na mke wake, kitendo kilicho sababisha mke wake kuuwawa na kumuacha mjane na pia kuwaacha watoto wake yatima bila mama.

Wachunguzi walisema kuwa uchambuzi wa simu ya Kori ulionyesha wakati wa mauaji hayo Joseph Kori hakuwa katika eneo la Juja bali alikuwa katika eneo la Ngong kaunti ya Kajiado.

Mume huyo wa mwendazake Mary aliweza kuwaambia polisi kuwa alikuwa na marafiki zake katika eneo hilo.

Polisi pia wanatarajiwa kupeana ripoti mahakamani kuwa polisi wa wanawake waliweka pilipili katika sehemu za siri za Judy kama alivyo dai mshukiwa huyo.

Kilicho fanya polisi waamini kuwa Kori hakuweza kuhusika katika mauaji hayo ni ujumbe mfupi ambao Kori alikuwa amemtumia Wambui saa nne usiku kuonyesha hakuwa nyumbani wakati huo.

Wawili hao wataweza kweli kupewa hukumu ya kuwafunza wananchi ambao wana tabia kama yao?

Inasemekana kuwa ujumbe huo ulikuwa unamwambia Mary aweze kulala kwenye alikuwa. Polisi waliweza kusema dereva huyo Michael Mathenge na Judy Wangui ndio washukiwa wakuu katika mashtaka ya mauaji hayo.