Marehemu arudishwa mochari kisa jeneza ya thamani ndogo

A coffin about to be lowered at a funeral service in a cemetery.
A coffin about to be lowered at a funeral service in a cemetery.
Baada ya jombi kuiaga dunia huko maeneo ya Narok, jamaa na marafiki walifanya kikao kuchanga pesa ya kumpa heshima zake.

Kama ilivyo desturi na mila katika familia nyingi nchini. Hadhi ya mwendazake ilikuwa ya juu sana na kwa hivyo walitakiwa kuchanga kiasi kizuri cha hela ili kuweza kumzika kiheshima. Inadaiwa kuwa alikuwa mwenyekiti wa chama cha wazee pale kijijini.

Watu walikusanyika na kuchanga pesa za kufadhili mazishi huku masharti yakiwa kununua jeneza ya hadhi ya mkubwa huyu. Inatokea kuwa jamaa aliyetumwa kununua jeneza aligawa kiasi cha pesa kwa mahitaji yake na kupelekea kununua jeneza ambayo wenzake waliirejelea kama sanduku tu.

Soma mengine hapa.

Mwili ulipofikishwa nyumbani ndani ya sanduku hilo, jamaa na marafiki walionekana kugutushwa na jinsi mwendazake anachukuliwa kimchezomchezo.

“Hii siyo jeneza bwana. Hii ni box !” mmoja wa waombolezaji aliteta.

Watu wa nyumbani walilazimishwa kurudisha jeneza hilo katika chumba cha kuhifadhi maiti ili waweze kununua jeneza ya hadhib ya mwendazake.

” Huwezi kumzika mkubwa na hiyo sanduku,’ mmoja alisikia akisema.