PATANISHO: Bwanangu hulala chumba tofauti akija nyumbani

Bi Tabitha, 46, alituma ujumbe akiomba apatanishwe na mumewe bwana Robert, 54, ambaye walikosana Disemba 2017.

"Mtoto alikuwa amekosea na nikamuadhibu na hapo mzee akakasirika na ikawa tu hatuelewani." Alisema Tabitha akidai kuwa mama mkwe ndiye alichochea kesi hiyo akidai kuwa amemuadhibu vibaya.

Baada ya Robert kuondoka Msambweni na kwenda Nairobi, mkewe bado yumo huko na kila mara wanapopatana kila mmoja hulala kwa chumba tofauti.

"Kama hataki turudiane anipate huku nyumbani anipeleke kwetu. Yeye hunishughulikia kila kitu ninachotaka bila tatizo lakini simu zangu huwa hajibu" Aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka 27.

Juhudi zetu za kumpata bwana Robert hazikufua dafu huku bi Tabitha asijue la kufanya.