Mwanamume azuiliwa kwa mauaji ya mwanawe wa miaka 10

crime_scene_tape
crime_scene_tape
Mwanamume anayetuhumiwa kwa mauaji ya mwanawe mwenye umri wa miaka 10 kwa madai ya kwenda haja kubwa ndani ya nyumba katika mtaa wa Kayole amezuiliwa kwa siku 10 huku uchunguzi ukiendelea.

Daniel Odongo anadaiwa kumuua mvulana huyo kwa kumpiga na kumjeruhi vibaya. Polisi wanasema mshukiwa amekuwa akiishi na marehemu.

Afisa anayeongoza uchunguzi Edward Mlanda ameambia mahakama kuwa mnano tarehe 16 Mwezi Mei, Odongo aliyekuwa akiishi na mwanawe anaaminika kumpiga vibaya mvulana huyo na kumsababishia majueraha tumboni.

Inadaiwa mvulana huyo alikula chakula kibovu na kupataka matatizo ya tumbo na kwa sababu alikuwa pekee yake alishindwa kutoka nje usiku na kulazimika kwenda haja ndani ya nyumba. Pia alitapika ndani ya nyumba.

 

Mvulana huyo alikuwa amefariki alipofikishwa katika hospitali ya Wilmad.

Mlanda alisema Odongo alitiwa mbaroni siku hiyo na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Kayole.

“ Sijakamilisha uchunguzi wangu na nahitaji muda zaidi ili kurekodi taarifa za mashahidi na kupata ripoti ya upasuaji wa mwili,” taarifa ya uchunguzi ilieleza.

Hakimu mkuu wa Makadara alikubali ombi la upande wa mashtaka na kuwapa polisi muda zaidi kukamilisha uchunguzi.

Kesi hiyo itatajwa Juni 3.