ILIKUAJE: Roho ya kifo ilifuata familia yetu - Evelyne Muthoka

Mwanadada kwa jina Evelyne Muthoka, ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje ndani ya kipindi cha Bustani la Massawe.

Evelyne ana story moja ya kugusa moyo sana kwani alisimulia jinsi katika familia yao ya watu kumi na wawili, wote walivyofariki na kubaki pekee yake. Cha kuhuzunisha ni kuwa wote walifariki katika mda wa miaka saba pekee.

Kulingana na Evelyne, anaamini kuwa roho ya kifo ilikuwa imeandama familia yao lakini mungu ndiye aliyemuokoa.

Mwanadada huyo ambaye sasa ni msanii wa nyimbo za injili, alizaliwa katika kitongoji duni cha Nyalenda katika familia ya watoto kumi, wasichana sita na vijana wanne.

Alieleza kuwa babake mzazi alifariki mwaka wa 1999 baada ya kuugua kifua kikuu na mamake akafariki mwezi uliofuata na kuwaacha yatima.

Baada ya kifo cha mama yao mzazi hapo msururu wa vifo katika familia yao ukaanza huku ndugu zake wakifariki kwa njia tatanishi. Isitoshe wanadada ambao walikuwa wameolewa pia waume zao walifariki kwa njia ile ile.

Soma usimulizi wake,

Mwaka wa 1999 Januari, baba alifariki kwani alikuwa anaugua kifua kikuu, na kwa sababu walikuwa wanapendana sana na mamangu, Februari mama akafariki.

Mwaka wa 2000 dadangu mkubwa akafariki mwezi wa Januari tarehe 5 baada ya kuugua. 2001 dada zangu wawili Rosemary na Ruth nao wakafariki. 

Rosemary alikuwa amelazwa hospitalini naye Ruth akawa mgonja. Ruth alifariki mikononi mwangu nikimtayarisha nimpeleke hospitalini.

Siku ya mazishi tukimuendea Rosemary ili twende mazishi ya Ruth nikapigiwa simu kuwa ameaga dunia.

Isitoshe, mke wa nduguye naye alifariki na ndugute akaamua kuoa mke mwingine, ndugu yangu akafariki na kumuacha mkewe ambaye alifariki baadaye.

Roho ya kifo ilituzunguka na wakati ilifika zamu yangu nikaambia mungu siwezi fariki kwani wote wakija kufariki nilikuwa namjua mungu.

Aliongeza,

Nduu ganyu Moses alikuwa mgonjwa na apotoka hospitalini, nilielekea kule kumchukua na baada ya dakika tano nilipigiwa simu eti amefariki.

Betty naye alikuwa amesombwa na mafikira wengi kwani watoto wengi takriban 17, walikuwa chini ya ulinzi wake na alikuwa amedhoofika moyoni.

Wakati aliliuliza dadake ako aje na kugundua kuwa amefariki, aliuliza ni saa ngapi na hapo akaaga.

Evelyne alisimulia jinsi siku moja alipokuwa ameelekea kuwazika dada zake alivopokea bahasha ambayo iliyokuwa na barua kutoka kwa bwanake akimpa talaka.

Ndani ya barua ile, bwanake alimwambia kuwa anajua kuwa dada zake wakifariki hufariki na waume zao na hataki kufariki pia.