Staa Willy Paul na Nandy wafunguka baada ya ajali

60321189_437838927008443_3214386645514881318_n
60321189_437838927008443_3214386645514881318_n
Safari ya kufika katika fiesta ya staa wa muziki wa kike Nandy kutoka nchi jirani ya Tanzania imepata mkosi baada ya gari lililobeba madensa, viongozi wa bendi kubingiria mkonani Morogoro na kusababisha majeraha makubwa.

Staa huyu alikuwa amesafiri na mastaa Willy Paul, BillNass Stamina, Juma Nature kuwakilisha na burudani hatari katika fiesta yake mkoani Sumbawanga.

Soma uhundo kamili:

Kufikia sasa hakuna anayedaiwa kufariki ila walioumia wamekimbizwa hospitali kupata matibabu. Staa Willy Paul amefunguka katika mtandao wake maridhawa wa insta na kusema kuwa wapo freshi.

"Tupo hai. Ni kweli kumekuwa na ajali ila hakuna ripoti ya mtu ameaga." asema Pozze.

Nandy katika kipande kifupi cha video amefunguka na kueleza kilichofanyika.

Soma hadithi nyingine hapa:

"Najua kuna taarifa zimezagaa mitandaoni kuhusu swala la ajali. Natoa wasiwasi kwa mashabiki wetu kuwa tupo vizuri. Gari iliyobingiria ni ya viongozi, madensa na watu wengine." amefunguka Nandy.

Msafara huu wa mastaa wa muziki unalenga kutikisa burudani katika mkoa wa Sumbawanga. Nandy amehakikishia mashabiki na wafuasi wake kuwa wapo njiani Iringa kuelekea Sumbawanga.