Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu Tarehe 13 Juni 2019

Yaliyomo katika bajeti iliyosomwa leo na waziri Henry Rotich 

SERIkali itatumia shilingi bilioni  326  kwa idara za usalama  mwaka huu wa kifedha .waziri wa fedha Henry Rotich  amesema usalama wa kitaifa ni nguzo muhimu sana katika kuhakikisha  uthabiti wa kiuchumi  na kuwavutia wawekezaji

 Kwingineko serikali imeitengea tume ya kupamabana na ufisadi shilingi biloni 2.9 na shilingi bilioni 3 kwa  afisi ya DPP ili kupiga jeki vita dhidi ya rushwa .waziri wa fedha Henry Rotich  amesema shilingi bilioni 5.7 zitakabidhiwa afisi ya mkaguzi mkuu wa mahesabu ya Umma .

  Hospitali ya kitaifa ya Kenyatta imetngewa shilingi bilioni 14.4 ili kuboresha huduma zake kwa wananchi ..waziri Henry Rotich pia ameitengea hospitali ya rufaa ya Moi shilingi bilioni 9.2 .

  Ajenda kuu nne za rais uhuu Kenyatta zimetengewa  shilingi bilioni 450 katika bajeti ya mwkaa wa kifedha wa 2019/20 .waziri wa fedha Hnery Rotich  amesema mgao huo ni pamoja na shilingi bilioni 47.8 za mpango wa afya ya gharama ya chini   UHC ambao pia umepata shilingi bilioni 7.9 kutoka hazina ya spoti na sanaa

Kampuni za michezo ya bahati nasibu zimepata pigo baada ya kuongezwa kodi nyingine ya  asilimia 10.waziri wa fedha henry Rotich amesema hatua hiyo imechukuliwa kuwazuia vijana kushiriki michezo ya bahati nasibu .

  NTSA yazipokonya leseni shule 51 za Udereva 

 Maamlaka ya NTSA imefutilia mbali leseni za kuhudumu za shule 51 za udereva ambazo zilikosa kuwasilisha stakabadhi za kupewa leseni mpya .shule hizo zipo katika  kaunti 16  na hazitaweza kupata huduma za NTSA mtandaoni .

Wachina 7 waliokuwa wakiuza mitumba Gikomba warejeshwa nchini mwao 

Raia saba wa  Uchina  waliokuwa wamefungua biashara ya kuuza nguo za mitumba katika soko la Gikomba wamerejeshwa nchini mwao .wizara ya usalama wa ndani imesema  watatu kati yao hawakuwa na vibali halali ya kufanya kazi nchini ilhali wanne  walijihusisha na biashara na shughuli za kujipa mapato kinyume na  matakwa ya vibali vyao.

 Jane Mariott  ndiye balozi ajaye wa Uingereza nchini Kenya

 Mtaalam wa kupambana na ugaidi  Jane Mariott ndiye balozi ajaye wa Uingereza humu nchini  kuanzia septemba mwaka huu . ataichukua nafasi ya Nic Hailey  ambaye amekuwa nchini tangu mwaka wa 2015 .

  wabunge na maseneta wakosa kuafikiana kuhusu mgao wa fedha za bajeti kwa kaunti

Kamati ya upatanisho kuhusu mswada wa ugavi wa mapato  imekosa kukubaliana muda mfupi kabla ya waziri wa fedha Henry Rotich kuisoma bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2019/2020 . utata umesababishwa na hatua ya maseneta kutaka kaunti zipewe  shilingi bilioni 327 huku wabunge wakisema shilingi bilioni 316 zitazitosha kaunti .

  Wakaazi wa kisauni wapata kituo kipya cha polisi 

 Wakaazi wa kisauni  wametakiwa kukitumia kituo kipya cha polisi  kilichofunguliwa katika eneo hilo ili kukabiliana na visa vya uhalifu .kamishna wa kaunti hiyo Evans Achoki  amewataka wakaazi  kushirikiana  na polisi kwa kuripoti visa vya uhalifu .

  Mtego wa Bomu la al shabaab wawauwa washukiwa 3 wa kundi hilo Boni

  Bomu la kujitengezea  ambalo  washukiwa al shabaab walikuwa wakilitega kando ya barabara  katika msitu wa Boni imelipuka na kuwauwa washukiwa watatu wa kundi hilo .polisi wanasema  bunduki tatu za AK 47  ni baadhi ya silaha zilizopatikana katika eneo la tukio .

Mbunge amshambulia mwenzake bungeni

Mbunge wa wajir mashariki Rashid  Amin ameshtumiwa kwa kumshambulia mwakilishi wa akina mama wa wajir   FATUMA Gedi katika majengo ya bunge mapema alhamisi .  kisa hicho kilifanyika katika eneo la kuegesha magari bungeni  wakati Bi.Gedi alipokuwa na  mwakilishi wa akina mama wa homabay  Gladys Wanga .

  Mbona wanwake hawaripoti dhlma za kijinsia ?

Woga ,fedheha ,ufisadi na utepetevu wa polisi ndio baadhi ya sababu ambazo huwafanya wanawake  kukosa kuripoti dhulma za jinsia . utafiti uliofanywa  katika mitaa ya mabanda hapa Nairobi  umeonyesha kwamba waathiriwa wengi waliwashtumu polisi na  maafisa wa utawala kwa kupokea rushwa kutoka kwa washukiwa  wa dhulma hizo

Mwathiriwa wa pili wa ebola aaga dunia Uganda 

Mwanamke mmoja raia wa Congo ndiye mgonjwa wa pili kuaga dunia nchini Uganda akwa ajili ya ugonjwa wa ebola . mwathiriwa huyo ni nyanyake  mtoto wa miaka mitano aliyeaga dunia hapo jana  baada ya kuvuka mpaka na kuingia Uganda kutoka DRC siku ya jumanne .

  Barabara zinazopakana na bunge kufungwa kwa ajili ya kusomwa kwa bajeti 

Tume ya uchaguzi na mipaka imeyaratibu majina ya watu kumi wanaozangatiwa kwa nafasi ya afisa mkuu mtendaji ili kuichukua nafasi iliyoachwa wazi na Ezra Chiloba . watatu kati yao ni wanawake  .tume hiyo imesema ilipokea maombi kutoka kwa  watu 90 .

Afisi ta DPP itawalinda mashahidi wote 

Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imetoa hakikisho kwamba itawalinda mashahidi wote  bila kujali kesi  ambazo mashahidi hao wanatumiwa kutoa ushahidi wao . Naibu mkurugenzi  Edwin Okello  amesema kila mtu  anayeripoti uhalifu ana haki ya kulindwa  na idara hiyo .