UKATILI! Yaya ahukumiwa maisha jela kwa kumbaka na kumwambukiza mtoto wa miaka 6 ugonjwa wa zinaa

Yaya mmoja huko Rongo amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumbaka na kumwambukiza mvulana mwenye umri wa miaka 6  maradhi ya zinaa . Neema Matiko  mwenye umri wa miaka 22  amepewa hukumu hiyo na  hakimu mkuu wa Rongo  Raymond Langat  kwa kosa hilo alilotekeleza machi tarehe 30 mwaka huu .

Langat amesema amempa mtuhumiwa hukumu hiyo kali kwa kutumia vibaya maamaka yake kuhatarisha  maisha ya mtoto huyo licha ya kufahamu kwamba  alikuwa na maradhi ya zinaa .

Mtoto huyo amepewa matibabu ili kumzuia  kuamubukizwa  maradhi hayo . Akijitetea ,mtuhumiwa aliitaka mahakama  kumwonea huruma kwa sababu  kosa hilo lilikuwa lake la kwanza .  Hakimu  amesema ingawaje mtuhumiwa  ana haki ya kujitetea ili ahurumiwe ,kosa lake ni kubwa kuliko   sababu alizotoa ili kupewa msamaha .

Mtoto aliyebakwa , mamake na jirani  ndio waliotoa ushahidi ddhidi ya yaya huyo  huku ripoti kutoka afisa wa matibabu ikithibitisha kwamba kweli mtoto huyo alidhulumiwa kimapenzi .