Baada ya Wema kufungwa jela, mamake Mondi atume ujumbe

sepetu
sepetu
Baada ya muigizaji na mwanamitindo kutoka nchi jirani ya Tanzania Wema Sepetu kufungwa gereza ya Segerea Dar, mamake mondi, Sandra Sanura Kassim ameonekana kuguswa sana na tukio hilo na kuchapisha picha katika mitandao ya kijamii akimtakia heri na utulivu wakati huu mgumu.

Pata Uhondo huu:

"Be strong my love..." alisema mamake Diamond Platnumz.

Tazama hapa:

https://www.instagram.com/p/By2XLfXhab9/

Wema alifungwa gerezani jana baada ya uamuzi ya mahakama ya Kisutu nchini humo kuamrisha atiwe nguvuni baada ya staa huyu wa kike kususia vikao viwili vya mahakama. Sepetu anaandamwa na kesi mbili. Kesi ya kwanza anayodaiwa kufanya ni kuchapisha picha na video za ngono katika mitandao ya kijamii.

Soma hadithi nyingine:

Wema aliieleza mahakama kuwa alijaribu kadri ya uwezo wake afike mahakamani ila kwa uchungu wa kuumwa na tumbo kwa sababu ya hedhi hangeweza kufika katika vikao hivyo vilivyoratibiwa Mei 11 na Juni 24.

Shtaka la pili ni kupatikana na dawa za kulevya aina ya marijuana. Wema atazuiliwa korokoroni mpaka juni 24 akisubiri dhamana ya kesi hizi mbili.

Dadake Diamond Platnumz, Esma pia ameonekana kuonyesha mapenzi na umoja wakati huu mwanamitindo huyu anapitia maisha magumu.

Tazama hapa:

https://www.instagram.com/p/By2Og6ogJOw/