Michael Joseph achukuwa nafasi ya Bob Collymore

MJ
MJ
Michael Joseph ameteuliwa kaimu afisa mkuu mtendaji wa Safaricom kufuatia kifo cha Bob Collymore. Kampuni hiyo imetangaza kwamba Joseph atashikilia wadhifa huo hadi pale bodi ya kampuni hiyo itakapotangaza afisa mkuu mpya wa kudumu.

"Bodi inaimani kwamba, Joseph atatoa muongozo na uongozi unaofaa wakati huu wa mpito,”," Katibu wa kampuni hiyo Kathryne Maundu alisema katika taarifa.

Michael Joseph alikuwa afisa mkuu mtendaji mwanzilishi wa kampuni hiyo kabla ya kustaafu na kumwachia majukumu Bob Collymore aliyefariki siku ya Jumatatu baada ya kugua saratani kwa kipindi cha miaka miwili.