Aliyekuwa mbunge wa Tetu, Githinji Ndung'u akamatwa na polisi

Aliyekuwa mbunge wa Tetu, Githinji Ndung'u alitiwa mbaroni jana usiku kwa madai ya uchochezi wa vurugu hapa jijini Nairobi.
Githinji anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo kuhukumiwa dhidi ya uchochezi na uharibifu wa mali ya wenyewe.
Githinji alikamata na maafisa wa polisi kutoka nyumbani kwake eneo la Kitisuru na kisha kupelekwa kwenye ofisi za maafisa wa flying squad kuhojiwa kabla ya kuwekwa gerezani.
Githinji anamiliki majumba kadhaa kule Kitsuru. Alikamatwa kwa madai ya kuchochea kundi la kigaidi kumvamia hakimu mmoja pamoja na wakaazi wa nyumba moja kwenye kijiji cha Kihingo, Kitsuru.
Githinji alikamatwa pamoja na Chacha Wabanga ambaye ni mfanyabiashara na mwanaume mwingine asiyejulikana. Hata hivyo, familia yake Githinji imemteta kwa kusema kuwa alikamata kwa madai ya kisiasa kwani alikuwa mwenyekiti wa kamati ya uhusiano wa kimataifa.
Kwingineko, washukiwa wawili wa wizi walipigwa risasi na maafisa wa polisi na kuliwa papo hapo kwenye mabishano baina ya polisi na wezi eneo la Westlands.
Washukiwa hao wanasemekna kuwa wakiwaangaisha waendesha bodaboda na abiria kwenye barabara kuu ya Waiyaki. Wakati polisi walijulishwa, washukiwa hawa walikuwa wanafanya uvamizi kwenye barabara hio eneo la Brookside.
Msemaji wa polisi eneo hilo ametaja kuwa walipata mali ya wizi huku maiti za wawili hao zikipelekwa chumba cha kuhifadhi maiti cha city.