Hatari: Unataka nyama?Cheki hii

Baada ya ufichuzi wa Runinga ya NTV kuhusu jinsi baadhi ya wafanyibiashara wanavyotumia kemikali hatari kuhifadhi  nyama na bidhaa nyingine zinazotengezwa kutumia nyama ,hizi hapa baadhi ya  ishara kwamba nyama unayonunua huenda imehifadhiwa kutumia kemikali  hatari ,au sio salama kuliwa .

1.Hakuna Nzi  

Iwapo wewe hununua nyama katika duka la nyama lakini hujawahi kuwaona  nzi wakipepea katika nyama ama sehemu inakouzuiwa ,huenda ni  daalili kwamba nyama hiyo imehifadhiwa kwa kemikali .Wengi hutumia kemikali iitwayo Sodium metabisulfite , ambayo wizara ya afya imesema  inafaa tu kutumia katika aina tofauti za bidhaa .kemikali hiyo pamoja na kemikali ya Formalin  imedaiwa kutumiwa na wauzaji wa nyama ili kuitunza isalie na ‘ubichi’ kwa muda mrefu  na huwaua nzi .Ishara ya kuwepo nzi ni thibitisho linalofaa kukupa hakikisha kwamba nyama hiyo haijahifadhiwa kutumia kemikali .  Wengi hufikiri kwamba hamna nzi kwa sababu ya usafi wa eneo hilo ,kumbe Lo! Kemikali huua nzi wote!

  1. Rangi ya Nyama

Baadhi ya nyama hasa mbichi huwa na rangi inayotambulika ya nyekundu lakini rangi nyekundu kupindukia huenda ni ishara ya matumizi ya kemikali kuihifadhi.baadhi ya kemikali hizo pia hugeuza rangi ya  nyama kuonekana  na madoadoa meusi .unafaa kuwa mwangalifu kuhusu rangi  ya nyama unayonunua .

  1. Harufu

Kila aina ya nyama  ina harufu inayotambulika .kwa mfano nyama ya ng’ombe huwa na harufu inayojulikana na wengi ambao hula nyama .mbuzi pia ina harufu yake.Lakini unafaa kuwa mwanaglifu endapo nyama unayonunua ina aina fulani ya harufu isiokuwa ya kawaida .huenda imehifadhiwa mahali paspofaa au kutumia kemikali .

4.Muhuri wa daktari wa nyama .

Hili halitiwi mkazo na wengi hasa  katika maeneo ya mijini.lakini inafaa kwa kila muuza nyama kuweza kuwahakikishia wateja kwamba nyama inayouzwa imekaguliwa na mtaalam . Hapa Nairobi imekuwa jambo la kawaida kwa watu kuuziwa nyama ambayo haijakaguliwa .mashambani ,watu hutumia ulaghai kwa kuchinja mifugo wenyewe na kisha kuichanganya nyama hiyo na ile iliyokaguliwa lakini hilo ni hatari sana kwa afya .wanyama huwa na magonjwa ambayo yanaweza kuambukizwa kwa binadamu .

  1. Kununua nyama ya bei rahisi

Najua wengi mmeshawahi kusikia usemi wa kawaida kwamba sehemu fulani huuza nyama kw abei ya chini .kuwa mwangalifu kuhusu vitu vya bei rahisi .Aghalabu nyama kama hiyo imepataikana kwa njia isio halali na huwezi kujua ilifikishwa vipi katika eneo inakouzwa . Hakikisha una eneo maalum au dula fulani unaloweza kutegemea kwa nyama unapoihitaji. Cheap is expesive.

 Mwongozo huu unafaa kuwa msingi kwako kuweza kutofautisha nyama ilio salama kwa matumizi ya binadamu lakini kuna njia nyingi za kuweza kufahamu hilo.