Maajabu! Jamaa akamatwa kwa kuuma masikio ya mpwa yake

masikio
masikio
Mwanaume mwenye umri wa makamu kutoka Muringene Igembe ya kati anazuilwa katika kituo cha polisi cha Maua akingoja kufikishwa mahakamani baada ya kuuma masikio ya mpwa wake.

“Nilikuwa natoka shuleni nikieleka nyumbani kula chakula cha mchana na nilipoingia kwa nyumba mjomba wangu aliuma masikio yangu mawili." Kijana huyo mchanga alieleza.

Kijana huyo Samuel Mwenda alisema kuwa hakukuwa na yeyote katika makazi hayo.

Isaiah Ntomburi ambaye ni babake kijana huyo wa miaka saba alisema nduguye alimfungia mwanawe kabla ya kuuma masikio yale. Alisema kuwa yeye na nduguye John Mutirithi ni watoto wa baba mmoja ila mama tofauti.

Wakazi wa eneo hilo bado wanashindwa kama hali ya akili ya Mutirithi iko sawa.

“Ana bahati sana kwani naibu wa chifu wa eneo hilo alikuwa karibu kwani wakazi wenye gadhabu walitaka kumuua." Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho alisema.

Inasemekana jamaa huyo alimfungia kijana huyo chumbani kabla ya kumuuma masikio baada ya kuchukua mfuko wa nyanyake ambao ulikuwa kwa nyumba ya mjombake.

Kijana huyo alipiga mayowe na majirani wakaja kumuokoa na kukimbilia shuleni baada ya Mutirithi kufungua nyumba. Wakazi wenye hamaki walimpiga mateke na mangumi na walitaka kumuua mshukiwa kabla ya naibu wa chifu kuingilia kati.