'Wakenya hawaimbi muziki wa Afrobeat,' Bien atetea Beyonce

Filamu ya Lion King imekuwa ikiongelewa juma iliyopita, huku wasanii wa Kenya wakisikitika kuwa hakuna hata mmoja wao aliyeonyeshwa kwenye wimbo wa sinema hiyo ulioimbwa na Beyonce.

Wengi wao walisema kuwa hadithi hiyo ilikuwa na msingi wa Kenya, angalau mmoja wao angekuwa kwa sehemu ya wimbo huo ili kusaidia kuelezea hadithi hiyo kwa njia ya kibinafsi.

Lion King anatumia kifungu maarufu cha Kiswahili, "Hakuna Matata", ambacho kilikuwa maarufu kwa wimbo wake John Katana,wa Jambo Bwana.

Amekuwa akipigania kupata hakimiliki ya kifungu hicho baada ya Disney kuchukua umiliki wa Hakuna Matata mwaka jana na sasa anashangaa kwamba hakuna msanii ata mmoja wa Kenya ambaye ameekwa kwa wimbo huo.

Wakenya wengi wamesema kuwa Sauti Sol wangekamilisha kanda hiyo. Lakini Bien mmoja wa waimbaji wa Sauti Sol alisema kuwa Beyonce akikuwa akiongozwa na Afrobeats ila wakenya hawafanyi muziki wa Afrobeat.

Aliendelea kusema kuwa,

Beyonce alikuwa akifanya albamu iliyoongozwa na Afrobeat na Wakenya hawafanyi muziki wa Afrobeat. Aina hiyo ya muziki hupatikana nchini Nigeria na Ghana, na ndipo alipoenda kutafuta wasanii.

Beyonce alisema alikuwa anatengeneza albamu yake itwayo 'The Gift', na kusema kuwa ilikuwa barua ya upendo kwa Afrika.

"Hii sauti ni barua ya upendo kwa Afrika, na nilitaka kuhakikisha kuwa tutapata talanta bora kutoka Afrika," alisema.

Soma mengi