Jamaa aliyejaribu kuvamia ikulu asema alitaka kuwaokoa vijana

Brian Kibet, aliyejaribu kuvamia ikulu ya Rais ameiambia mahakama kuwa alikuwa anajaribu kuwaokoa vijana wa Kenya kutokana na Janga la ukosefu wa ajira. Brian kwa sasa ni mwanafunzi chuo kikuu cha JKUAT.

Bera alipigwa Risasi na polisi wanaoweka doria katika Ikulu ya rais alipokuwa anajaribu kupenyeza ndani. Brian mwenye umri wa miaka 25 alieleza mahakama kuwa yeye ni mtu mzima na hivyo hahitaji kuchungwa na babaye mzazi kwani anauwezo wa kujifanyia maamuzi yake mwenyewe.

Pamoja na hayo, Brian alisisitiza kuwa hali yake ilikuwa shwari na hivyo hakuhitaji kurejea katika hospitali ya wagonjwa wa akili kwani angekosana na polisi pamoja na madaktari kwa haraka sana. Brian hata hivyo aliiomba mahakam kumsamehe kwani alikuwa ameapa kwamba hatarejea kwa tendo lingine kama hilo.

Hata hivyo, jaji Francis Andayi alikataa ombi hilo na kusema kuwa,"Mshtakiwa anahitaji kuchungwa pamoja na kupewa usaidizi kwa kunywa madawa yake. Pia, nimempata mshukiwa kuwa hayupo kwenye hali nzuri kuweza kuachiliwa na mahakam."

Brian kwa sasa yupo katika hospitali ya wagonjwa wa akili kwa miezi miwili na anatarajiwa kurudishwa mahakamani mnamo tarehe tisa mwezi Octoba. Awali, Brian alimwomba msamaha rais Uhuru Kenyatta kwa kitendo chake hicho.