"Mimi ni mtoto wa pili kwa familia ya watoto watatu. Wazazi wangu waliaga dunia nikiwa darasa la nne hivo ikatubidi tukalewe na nyanya yetu. Hata hivyo, hali ya taanzia ilizidi kuniegemea nilipofika darasa la saba wakati nyanya yetu pia alipiga dunia teke na hivyo tukabaki watoto mayatima."
Baada ya kifo cha walezi wake, Evans alibaki bila chaguo la maisha. Kulingana na Evans pamoja na vijana wengi mtaani Dandora, Wizi tu ndio uliokuwa njia ya kipekee ya kufanikiwa maishani hapa mjini Nairobi.
"Baada ya kifo cha wazazi nilibaki bila chaguo na ndipo nilijitosa katika shughuli nzima ya wizi. Nikiwa mtoto tulikuwa tunaona majambazi wakiwa na maisha mazuri pamoja na kuwa na wapenzi warembo kweli kweli. Kwangu mimi wakati huo nilikuwa naamini kuwa ili niweze kufanikiwa lazima niwe jambazi."
Hata hivyo, Ili Evans aachane na tabia ya wizi aliponea chupuchupu kupatana na mauti yake.
"Niliponea mara mbili kuangamizwa. Siku moja nilimwimbia mtu simu kisha akapiga nduru. Umati wa watu ulijaa eneo hilo na wakaanza kunipiga kwa mawe. Kabla hawajaniua, Polisi waliwasili eneo hilo na wakaninusuru kwa kunitia Pingu. Mara ya pili ilikuwa tarehe 24 mwezi disemba ambapo tulikuwa na marafikizangu watatu tukifanya uhalifu. Baada ya kuimba mali ya mtu binafsi kumbe wananchi walikuwa wanatufuata. Hapo nikaambia marafiki zangu waningoje niingie msalani."
Kifo cha marafiki zake kilimshtua sana jambo lililobadilisha maisha yake. Evans alianzisha shirika la kuwahamasisha vijana kuachana na wizi baada ya matukio hayo na sasa shirika hilo linafanya kweli mtaani Dandora.
"Kwa sasa niliachana na wizi na kazi yangu ni kuhamasisha vijana waachane na wizi.Iwapo mtu anakataa kutusikiliza basi sisi tunamwacha pamoja na kueleza askari ili waweze kuendele ana yeye sasa kutoka hapo."
Evans amemalizia kwa kuwapa vijana wadogo pamoja na wakenya wote ushauri anao amini kuwa utawasaidia watu wote."
"Vijana mjue kua wizi hauna faida kwa utajipata mahali kuwili pekee, Jela ama Kaburini na kabla haya yatokee si jamani ubadilike kwa sababu lipo jambo unaloweza kufanyia jamii. Wakenya nanyi mjihadhari na muache tabia ya kuweka simu zenu vibetini hasa wanawake kwani hilo huwa jambo rahisi kwa jambazi kukupokonya sim yako. Kwa kulinda majumba yenu,Mwombeni mwenyezi Mungu awasaidie ila nayi mnunue kufuli za maana."