ODM yawatema 9 nje ya mchuano wa ubunge Kibera. Nani yuko ndani?

unnamed (1)
unnamed (1)
Chama cha ODM kimewasilisha orodha ya majina 11 kati ya 20 ya wagombeaji katika uchaguzi mdogo wa ubunge Kibera. Hii ni baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi kufuati kifo cha Ken Okoth.

Tisa wametemwa nje baada ya kukosa kuafikia vigezo vya chama hiki. Idadi ya wagombea 23 waliojaza fomu imepungua hadi 11 sasa ili kujitayarisha kwa mchujo wa chama utakaofanyika Agosti 31 kabla ya uchaguzi utakaofanyika Novemba 7.

Soma hapa:

 Mwenyekiti wa bodi kuu Judith Pareno jumatatu wiki hii ametoa mwongozo kwa wawaniaji wa kiti hiki walipe elfu 200 pesa taslimu kabla ya saa sita jumanne ili kuzuia kufungiwa nje ya zoezi hilo.

Majina yaliyowasilishwa ni ya Christone Odhiambo almaarufu kama DJ Kris Darlin, Peter Ochieng, Tony Ogola Sira, Reuben Ojijo and Stephen Okello.

Bernard Otieno, Eric Ochieng, Brian Owino, John Otieno, Benson Musungu and Patrick Lumumba Owade ni majina pia ambayo yapo kwenye orodha.

Chama tawala cha Jubilee pia kinatarajiwa kutoa mgombeaji wao baada ya shinikizo katika chama hicho. Rais Kenyatta ambaye ni kinara wa chama hicho hakutaka wawasilishe mgombeaji ila baada ya wanachama kushauriana wakaamua kufanya hivyo.