Mama alimuuza mtoto wangu kwa shillingi 35,000

child
child

Wanawake watatu washtakiwa kwa kumuuza mtoto kawangware.

Kabla ya Judy kujifungua mtoto wake, hakujua kuwa mtoto wake alikuwa ameuzwa na mama yake tayari kwa shillingi 35,000, bei ambayo ni mama yake mwenyewe alikuwa ameiweka.

Judy alisema kuwa mama alikuwa anamhudumia vizuri sana akiwa na mimba bila yeye kujua kuwa alikuwa anafanya haya mambo yote ili akishajifungua mtoto wake salama, amuuze mtoto huyo na kupata pesa.

Binti huyu alipoenda kujifungua, mama yake alikuwa kando yake kwani, alikuwa amesema mwenyewe kuwa atampeleka Kenmed Clinic iliyo mtaa wa kawangware.

Judy aliwaambia polisi kuwa, alijifungua mtoto mrembo wa kike mwenye uzito wa kilo tatu.

"She offered to take me to Kenmed Clinic in Kawangware where I gave birth to a beautiful baby girl weighing 3.1 kilos,"

Hata hivyo, Judy hakujua kuwa mama yake alikuwa ameliandikisha jina lake kama jina la mwanamke aliyenunua mtoto. Mamake Judy aitwaye Shimuli, alikuwa anapanga njama hiyo ya kumtororsha na kuuza mtoto na mfanyikazi mmoja wa hospitali hiyo, Gertrude Mutende na mwanamke mwingine Joyce Musundi.

Joyce Musundi alikuwa amebeba mtoto huyu na kumpeleka mpaka Umoja pale ambapo aliyenunua mtoto aliishi.

Zaidi ya hayo, Judy alisema kuwa mama yake alimwambia anaeza kuenda nyumbani na amuache mtoto wake hospitalini akidai kuwa atakuja nyumbani na yeye. Judy bila kusita alimuamini mama yake na kumuacha na mtoto wake, pasi kujua mama yake alikuwa na mipango yake.

Kulingana na utafiti, inasemekana kuwa baada ya Judy kuenda nyumbani, Musundi alifika kwenye hospitali hiyo ,akalipa bili ya hospitali kisha akachukua mtoto wake Judy. Shimuli, nyanyake mtoto, alishika njia na kukutana na Musundi kisha wakaelekea mtaa wa Umoja kumalizia dili yao.

Walipofika umoja, mtoto huyu alipewa mnunuzi kisha Shimuli akapewa shilingi zake 35000.

Shimuli aliporudi nyumbani pamoja na Musundi bila mtoto wake Judy, Judy alijua kuwa kuna kitu kilichokuwa kinaendela kisha akaamua kumtumia shemeji yake ujumbe mfupi akimueleza yaliyotokea.

Papo hapo, shemeji yake alipeleka ripoti kwenye kituo cha polisi na baada ya uchunguzi wa mapolisi kufanywa, Shimuli, Musundi na Mutende walitiwa mbaroni na polisi na kuwekwa mbele ya mahakama ya Kibera.

Watatu hawa walihukumiwa na hakimu Joyce Gandani aliyewaambia walipe dhamana  ya shillingi 100,000.

Aliyemnunua mtoto anazazidi kutafutwa kwani alijificha asije akafungwa  gerezani pia.

Kesi hii itaskizwa kutoka tarehe 7, mwezi wa Disemba.

Ama kwa hakika, umdhaniaye siye, ndiye!