Diamond aombwa kuvunja Wasafi Festival Iringa. Mwakyembe aeleza

mond
mond
Staa na nyota wa Afrika Diamond Platnumz ametakiwa kuifutilia mbali tamasha la Wasafi mjini Iringa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amemtaka mkali huyu wa Inama kuuweka utaifa mbele na kuhudhuria tamasha litakalofanyika nchini humo la JAMAFEST.

Soma hadithi nyingine:

Staa huyu hajaweza kujibu ombi hilo.
Mwakyembe amemuomba msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kubadilisha ratiba ya Wasafi Festival mkoani Iringa ili ahudhurie kwenye tamasha la kizalendo la JAMAFEST.

JAMAFEST ni fiesta inayokusanya mataifa yaliyo katika ukanda wa Afrika Mashariki .

Tamasha hili linatazamiwa kuwavuta mastaa wengi wa muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Waziri Mwakyembe akizungumza na vyombo vya habari nchini humo amemtaka Mondi kufuata agizo hilo.

Soma hadithi nyingine:

"Nimempigia simu kijana wetu nyota wa muziki barani Afrika na pia ulimwenguni ukipenda. Nikamueleza kwamba sasa huu ndio muda wa kuonesha utaifa." Amesema waziri Mwakyembe.

Mwakyembe anamtaka staa huyu kuvunja ziara ya Iringa kwa sababu ya uzalendo wa taifa hilo.

Tamasha hili litafanyika kati ya Septemba 22 hadi 28 mwaka huu