(+ Picha) Baba, mwana na mjukuu wafariki katika hali tata Machakos

Wingu nzito la simanzi limegumbika familia na kijiji  kimoja kaunti ya Machakos baada ya wanafamilia watatu kuaga ghafla.

Familia ya Samuel Mutunga almaarufu kama Uncle Sam inasikitika kumpoteza.

Soma hadithi nyingine:

 Sam ni mtu mashuhuri na muuzaji mkubwa wa fenicha kaunti hiyo.

Mwanawe na mjukuu wake Samuel wamefariki dakika chache baada ya mwendazake kuaga.

Samuel alitangulia kupoteza uhai wake baada ya kuanguka na kuzirai nyumbani kwake Katheka Kai.

Mwendo wa sasa tatu unusu, Roy Mwendwa alifariki baada ya kugonga matatu ya abiria 14.

Soma hadithi nyingine:

 Mjukuu wa Samuel aliyekuwa katika gari hili ameaga dakika chache katika Hospitali ya Machakos Level 5.

"Mwendwa alikuwa anasafiri na gari lake Toyota Mark II (KBR 906A) kutoka mji wa Machakos. Ndani alikuwa na binamu na mtoto wake alipogongana na matatu ya Makos Sacco KBN 256R..."  Kamanda wa Trafiki Harriet Kathure.

Dereva wawili wa gari hizo wameaga papo kwa hapo.

Abiria wa matatu wamekimbizwa hospitali ya Machakos Level 5 kwa huduma ya kwanza.