James Ng'ang'a ampiga vijembe Snoop Dogg, ampa onyo kali ( + Video)

ggg__1569489080_71959
ggg__1569489080_71959
Mhubiri wa kanisa la Neno Evangelism Centre Jame's Nga'ng'a amemjibu rapa na staa wa Marekani Snoop Dogg kuhusu video.

Katika video fupi inayosambaa katika mitandao ya kijamii, kasisi huyu anatoa kauli kuhusu Snoop Dogg ,

"Naskia nimetajwa na Watch doggi…Snufu Dog, Sniff Dog, ni mtu mmoja kama Michael Jackson. Naskia aliweka hiyo akapata comment more than 1 million, akatoa. We Snoop Dogg imba nyimbo zako za kimataifa, wachana na Ng’ang’a. Wakamba wanasema Ukamanya."

Soma hadithi nyingine:

https://www.instagram.com/p/B21pDJVlU0d/

Snoop Dogg aliteka mitandao ya kijamii mapema wiki hii baada ya kuchapisha video ya Ng'anga katika mtandao wake wa Insta.

Baadaye rapa huyu aliitoa video hiyo katika akaunti yake ya Insta.

Katika video hii, James Ng’anga anaonekana akiwazaba makofi waumini kanisani katika ibada inayopeperushwa katika runinga ya Sasa.

Haya yanajiri muda mchache baada ya muhubiri huyu kusema kuwa wanaosambaza video zake ni Ibilisi wanaotaka kumshusha

Ng’ang’a anahoji kuwa video zile ni za maadui wanaolenga kumshusha na kumchafulia jina.

“Huwa nafanya mambo mengi mazuri. Nawapa watu chakula, lakini hao wanakata tu (video)  ile nimeongea vibaya kwa sababu ni watu wana mapepo.” Alisema Ng’ang’a.

Kulingana na rapa huyu, hivi ndivyo kasisi anavyopaswa kumwadhibu mtu sadaka inapokosa kutoshea.

Soma hadithi nyingine:

Asichoelewa Snoop Dogg ni kuwa tendo la kuwazaba kofi waumini ni njia moja ya kufanya ibada.

Ng'anga sasa anamtaka Snoop Dogg kumakinika katika kazi yake ya kutumbuiza na kumkoma kabisa.