Je Jaguar amwinda Lulu Diva? Mwanamuziki apasua mbarika

Lulu-Diva-2
Lulu-Diva-2
Mwanamuziki kutoka Tanzania, Lulu Diva amefunguka kuhusu uhusiano wake na mbunge wa Starehe, mheshimiwa Charles “Jaguar” Njagua.
Kupitia mahojiano ya moja kwa moja, Diva alimuambia mwanahabari wa Tanzania Diva The Bawse  kuwa Jaguar amekuwa akimmezea mate na pia yeye amekuwa akimvizia vizia Jaguar.
HATUJATENGANA KWA SABABU MIMI NAYE HATUJAWAHI KUWA NA UHUSIANO WOWOTE.

Aliongeza kuwa,

AMEKUWA AKINIVIZIA NAMI NIMEKUWA NIKIMMEZEA MATE. KWA HIVYO SISI SOTE TUNATAMANIANA TU NA TUKAAMUA KUWA WACHA MAMBO YAWE HIVYO.

Hapo awali, ilikisiwa kuwa Lulu alikuwa anachumbiana na aliyekuwa mmoja wa kikundi cha muziki cha Wasafi records, Rich Mavoko.

Hata hivyo, hivi majuzi yeye na Diamond Platnumz wamekisiwa kuwa kwenye uhusiano, madai ambayo mkuu huyo wa WCB alikana.

Alipoulizwa kama anatarajia kujifungua mtoto wa aidha Jaguar au Diamond Platnumz, Diva alikana akisema;
LA HASHA SINA MIMBA.