Yaliyomo: Hali tete Kakamega, jumba laporomoka na kuua watu (+Picha)

Nyuma ambayo ipo kwenye ujenzi imeporomoka na kuua watu Butali Kakamega.

Idadi ya watu wawili wameaga baada ya jumba la ghorofa mbili kuporomoka katika kaunti ya Kakamega.

Kisa hiki kimefanyika soko ya Butali leo Alhamsi.

Soma hadithi nyingine;

Idadi ya manusura haijulikani huku ikikisiwa kuwa huenda kuna watu wengi waliosalia kwenye vifusi vya jumba hilo.

Msaada wa huduma ya kwanza umepatikana kutoka kwa wahudumu wa msalaba mwekundu na wanakijiji waliokuwa wa kwanza kushuhudia kisa hicho.

Kwa mujibu wa walioshuhudia kisa hiki, sampuli ya changarawe iliyotumika katika ujenzi imechangia kisa hiki.

Naibu gavana wa Kakamega Philip Kutima amehakikishia wananchi kuwa hali iko sawa na serikali ya kaunti itashughulikia swala hilo.

Amedokeza kuwa zoezi la kuwatoa waliokwama ndani imeanzishwa.

Soma hadithi nyingine;

Miili ya wafu imesafirishwa kwa ufadhili wa serikali ya kaunti na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha Malaba.

Taarifa za hivi karibuni zinaonyesha kuwa watu 7 bado wapo kwenye vifusi vya jumba hilo.