Musalia Mudavadi aahidi kuwania kiti cha urais 2022

Musalia-compressed
Musalia-compressed
Kiongozi wa chama cha Amani National Congress Musalia Mudavadi amesisitiza kwamba atawania kiti cha urais katika uchaguzi mkuu 2022.

Mudavadi amesema amekuwa kwenye mashindano awali na atapambana hadi ashinde kiti hicho.

"Ningependa kuwahakishia wafuasi wangu kwamba nipo uwanjani na nitapambana hadi mwaka 2022. Nitakuwa debeni na sina shaka kuhusu hilo," Musalia alisema.

Alisema hayo Alhamisi katika chuo kikuu cha Masinde Muliro kwenye halfa ya matanga ya Adelaide Khalwale ambaye alikuwa mkewe Boni Khalwale.

Musalia alikuwa akijibu Khalwale ambaye alimsihi aungane na viongozi kutoka maeneo mengine ili kuunda serikali katika uchaguzi wa 2022.

Khalwale alisema kwamba ni vigumu sana kwa Mudavadi kufikia kileleni bila kuungwa mkono na viongozi kutoka maeneo mengine huku akisema kwamba kuwa rais katika taifa hili inagharimu sana.

"Kwa sababu mimi ni kiongozi anayeheshimiwa katika jamii yangu, nimechukua hatua ya kwanza kwa kufanya urafiki na wanaziaza maarufu kutoka maeneo mengine, kaunti nyingine, ilii kuunda utaratibu wa serikali ijayo. Hakuna njia ya mkato," Khalawale alisema.

Khalwale ambaye anafahamika kuwa mfuasi mkubwa wa Naibu wa Rais William Ruto anawajibikia jamii ya Luhya iliyoungana na kwa sasa yeye ni mfuasi mkubwa wa Mudavadi hata kuliko 2013.